WADAU WA KILIMO NA USTAWI WA JAMII WAKUTANA DODOMA
Na. Siza Kangalawe,
Habari - DODOMA RS
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya ameongoza kikao kazi cha wadau wa kilimo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la 'Community Development Initiative Support (CDIS)' lenye dhamira ya kujenga mabadiliko chanya na kuhakikisha ustawi wa jamii.
Kikao hicho kimewajumuisha Seksheni ya kilimo ngazi ya Mkoa pamoja na Mkurugenzi wa CDIS Bw. Joseph Laizer na timu yake,lengo likiwa ni kutambulisha mradi wa "Imarisha Fursa za Ajira kwa Vijana" ambao unaotarajia kufanyika kwa muda wa miezi 36 katika mikoa ya Dodoma na Morogoro ,ambapo bajeti ya Utekelezaji wa mradi huu kwa Mkoa wa Dodoma ni Dola za kimarekani 98,750, kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Oktoba 25/2024.
Comments
Post a Comment