WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA
Na Sofia Remmi
Habari-Dodoma Rs
Katibu tawala mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar K.Mmuya ameongoza hafla ya chakula cha pamoja kwa watumishi wake,ambapo kama ilivyo ada, hafla hiyo imekwenda sambamba na kusherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa watumishi waliozaliwa mwezi Oktoba.Hafla hiyo imefanyika Leo tarehe 31 Oktoba 2024.
Aidha katika hafla hiyo watumishi walipata mafunzo ya afya ya akili kutoka kwa msaikolojia wa Hospitali ya Taifa ya Akili (Mirembe) Bi.Gaudensia Kalalu.
Msaikolojia kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Bi.Gaudensia Kalalu, akitoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma kuhusu namna mtu anavyoweza kuathirika na changamoto ya afya ya akili.
Comments
Post a Comment