BENKI YA NMB YAKABIDHI KOMPYUTA 10 KWA MKUU WA MKOA WA DODOMA
Na; Happiness E. Chindiye
Habari - Dodoma RS
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Leo Novemba 28,224 amepokea Kompyuta 10 kutoka Benki ya NMB Mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya Benki hiyo kurudisha kwa jamii (CSR).
Kompyuta hizo zitatolewa kama motisha kwa walimu ambao Shule zao zimefanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani kwa shule za Msingi na Sekondari.
Walioshiriki kushuhudia makabidhiano hayo ni baadhi ya walimu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
#keroyakowajibuwangu
#Dodomafahariyawatanzania
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment