CCM YAHITIMISHA KAMPENI ZAKE KATIKA KATA YA MRIJO - CHEMBA










Na. Hellen M. Minja,
       Ha sobari – DODOMA RS


Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, leo Novemba 26, 2024, kimehitimisha rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 katika viwanja vya Kata ya Mrijo, Wilaya ya Chemba.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo wakati wa zoezi la kufunga Kampeni hizo, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Gavu, aliyekuwa mgeni rasmi amesema;

“Lazima tutulie sana na tufanye maamuzi yenye faraja na manufaa kwa ajili ya vizazi vyetu. Jukumu letu kwenu ni kuhitaji amani upendo na utulivu, jukumu la kuleta maendeleo tunalipenda. Chama chetu kina amini jukumu la uongozi ni kuwatumikia wananchi na si mtu mwenyewe” Ndugu Gavu

Akitoa takwimu za idadi ya wagombea waliojitokeza na waliopitishwa na Chama hicho wakati wa mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali, Katibu wa CCM Mkoa Ndugu Pili Mbanga amesema;

“CCM ilipata wagombea 29,447 ambapo wanaume ni 20,875 na wanawake ni 8,572. Jumla ya wanachama walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali ni 17,527 huku wanawake walioteuliwa katika mitaa na vijiji ni 44 huku jumla ya walichaguliwa katika vitongoji ikiwa 397. Vijana waliojitokeza kugombea nafasi ni 621. Mkoa unaendelea kusimamia ilani ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi” Ndugu Mbanga

Mbunge wa jimbo la Chemba Mhe. Mohamed Moni, amesema Kata ya Mrijo ndiyo imepata fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo elimu na afya.

“Katika Kata iliyopata fedha nyingi kutoka Serikali kuu lakini pia katika mapato ya ndani ni Kata ya Mrijo. Tumepokea zaidi ya Bilioni 3 kwenye elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyogharimu Shilingi MIlioni 540, zaidi ya shilingi Milioni 140 kukarabati shule ya zamani pamoja na shule 2 mpya za msingi. Tumepata Zahanati mpya mbili (2)” Mhe. Moni

Kadhalika, Katibu Mkuu UWT Ndugu Suzan Kunambi, ametoa hamasa kwa wanawake kujitokeza kwa wiki wakiambatana na familia zao siku ya Jumatano Novemba 27, kupiga kura za ndio kwa chama cha Mapinduzi kwani ndicho chenye kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.

“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”

 
#kurayakosautiyako               
#ujanjanikupigakura               
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu










 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA