DODOMA KUNA FURSA NYINGI ZA UWEKEZAJI,WAWEKEZAJI NJOONI MUWEKEZE : RC SENYAMULE
Na; Happiness E. Chindiye
Habari - Dodoma RS
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary S. Senyamule usiku wa tarehe 23.11.2024 ameshiriki uzinduzi wa 'LC Luxury Apartaments' mpya za kisasa zilizojengwa ndani ya Jiji la Dodoma.
Akizungumza na halaiki iliyojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza ndani ya Jiji hili, kwani kuna fursa nyingi ambazo zimeletwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tunampongeza kwa yote anayoyafanya ndani ya Mkoa wa Dodoma ya kutaka wageni wa hadhi zote wanaokuja kupata sehemu ya kupumzika kutokana shughuli zinazofanyika Jijini hapa, hivyo nitoe wito kwa wawekezaji wengine kuja kuweza Dodoma” -Mhe. Senyamule
#kurayakosautiyako
#ujanjanikupigakura
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment