MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA YAFUNGULIWA DODOMA













Na Sofia Remmi.
Habari -Dodoma Rs

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Asina Omari ambaye pia ni Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania, amefungua mafunzo kwa Watendaji Ngazi ya Mkoa ya  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura Leo tarehe 30 Novemba 2024.

Mafunzo hayo ya siku 2  yanayoongozwa na Kaulimbiu ”Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi bora”,yanalenga  kuwajengea uwezo wa kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata na kuhusisha namna ya ujazazi wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura, yamefanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ( Jengo la Mkapa)

Wakurugenzi wa Halmashauri za Chemba,Kondoa Mji na Kondoa DC, ni miongoni mwa Washiriki wa Mafunzo hayo ambayo yatahitimishwa tarehe 01.12.2024.

#kurayakosautiyako
#birthdayyangumtiwangu.










 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA