RAIS AMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WATU WENYE ULEMAVU.





Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule (Kushoto) akipokea Tuzo kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na uratibu) Mhe. Ummy Nderiyananga kwa ajili ya kutambua ushiriki wake kwenye chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Jakaya kikwete Conection Jijini Dodoma.









Na; Sofia Remmi.
       Habari - Dodoma RS

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amempongeza  Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi katika Sekta ya Elimu,ambayo lengo lake ni kuhakikisha watu wenye Ulemavu wanapata elimu bila vikwazo.

Mhe. Nderiananga ameyasema hayo  leo Novemba 24, 2024 wakati wa hafla maalumu ya chakula cha pamoja na Watu wenye Ulemavu iliyoandaliwa na 'Tanzania Foundation For Excellence in Disabilities' (tfed).

Akizungumza wakati wa hotuba yake,Mhe. Nderiananga Amesema kuwa Mhe. Rais ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia,sambamba  na kutoa mikopo  ili kuhakikisha kuwa Watu Wenye Ulemavu wanajikwamua kiuchumi.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia iko pamoja na Watu Wenye Ulemavu, ndio maana imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu ya shule Ili kuhakikisha wanapata haki ya elimu kama watu wengine "Mhe. Nderiananga.

Ameongeza kuwa  Serikali imeendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kupitia Halmashauri ambapo na Watu Wenye Ulemavu wamekuwa wakinufaika kwa kiasi  kikubwa.

Katika hatua nyingine Mhe Nderiananga,amekabidhi Laptop 45, vishikwambi 35,  fimbo nyeupe  200 magongo 100, Baiskeli 20 majiko ya gesi 400 na Vitimwendo 20 ambavyo vimetolewa na Taasisi inayoshughulika na masuala ya watu wenye Ulemavu (tfed).

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amesema Rais Dk Samia ameendelea kuwajali na kuwaenzi watu wenye Ulemavu kwa namna mbalimbali.

"Mheshiwa Rais ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kujenga shule za watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha kundi hili linapata fursa ya kupata elimu bila vikwazo.

Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa watu wote ikiwemo wenye Ulemavu lengo ni kuhakikisha wanashiriki katika shughuli za uzalishaji na kujikwamua kiuchumi," Mhe. Senyamule.

Mhe. Senyamule ameongeza kuwa  mwaka huu wa fedha Halmashauri tano zimetenga sh.milioni 19 kwa  ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa watu Wenye Ulemavu. Niwahakikishie kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kundi hili linaendelea  kuishi sawa na Watu wengine,"alisema

 Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma (SHIVYAWATA) Omary Lubuva  amewashukuru wadau kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaunganisha pamoja kupitia shughuli mbalimbali.

#kurayakosautiyako
#ujanjanikupigakura
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu












 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA