"SERIKALI YETU INATAKA UCHAGUZI WA AMANI NA UTULIVU" - RC SENYAMULE
Na; Happiness E. Chindiye
Habari - Dodoma RS
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amesema Serikali inataka uchaguzi wa amani ,utulivu ,haki na demokrasia,na kwamba Serikali ya Mkoa imejipanga kuhakikisha maelekezo hayo yanafuatwa.
Akizungumza na kundi la Vijana Novemba 23,2024 katika mashindano ya Mdahalo wa Vyuo uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba, Mhe. Senyamule amesema,
“ Serikali yetu inataka uchaguzi wa Amani na utulivu Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan mmemsikia mara zote anataka haki na demokrasia sisi kama Serikali ya Mkoa wa Dodoma tumejipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki,amani na utulivu.Kwa kufanya hivyo, itatuongezea mshikamano,Utaifa wetu na umoja kama Watanzania”
Mashindando hayo ya Mdahalo wa vyuo yaliongozwa na mada ; Ukosefu wa Uzalendo miongoni mwa wananchi huchangia ushiriki hafifu wananchi katika uchaguzi.
#kurayakosautiyako
#ujanjanikupigakura
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment