WATANZANIA 26,963,182 WAMEPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA : WAZIRI MCHENGERWA
Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Jumla ya Watanzania 26,963,182 ( Milioni ishirini na sita,laki tisa,elfu sitini na tatu,mia Moja themanini na mbili) wenye sifa za kupiga kura, wametimiza haki yao ya Kikatiba kwa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, uliofanyika Nchini kote mnamo Novemba 27, 2024.
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) Novemba 28, 2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, jengo la Mkapa Jijini Dodoma alipokua akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mbele ya Waandishi wa Habari.
“Jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha, kati yao wanawake ni 16,450,559 na wanaume walikua 15,236,772. Wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikua ni 31, 255,303. Aidha wananchi waliopiga kura siku ya tarehe 27 /11/2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokua na sifa ya kupiga kura”. Mhe. Mchengerwa
Aidha, aliutangazia Umma matokeo ya jumla ya Uchaguzi huo.
“Nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji, maeneo yaliyofanya uchaguzi ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na 99.01%, CHADEMA imeshinda nafasi 97 sawa na 0.79%, ACT WAZALENDO imeshinda nafasi 11 sawa na 0.09%, CUF imeshinda nafasi 10 sawa na 0.08%, NCCR MAGEUZI imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01%, UND imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01% na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na 0.01%”.
Hata hivyo,kutokana na baadhi ya maeneo kushindwa kufanya uchaguzi kwa sababu mbalimbali ikiwemo vifo,Mhe. Mchengerwa amesema yatapaswa kuzingatia kanuni za Serikali ili yaweze kufanya uchaguzi na kupata Viongozi wao, na amevishukuru vyama vyote vilivyoshiriki Uchaguzi huo.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki”.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment