WATUMISHI RS DODOMA WASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA PAMOJA NOVEMBA
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Novemba 29,2024 wamekutana kula chakula cha pamoja na kusherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa Watumishi waliozaliwa mwezi Novemba,ikiwa ni utaratibu wa kawaida uliowekwa na Uongozi kwa kila mwezi.
Kama ilivyo ada,baada ya chakula na kusherekea kumbukizi za kuzaliwa,Watumishi hao walipatiwa mafunzo,ambapo mada tatu ziliwasilishwa ambazo ni Itifaki,Lishe na Mtindo Bora wa Maisha pamoja na Umuhimu wa Mazoezi kwa Afya.
#birthdayyangumtiwangu
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
Comments
Post a Comment