RC SENYAMULE ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA NA WENYE MAHITAJI.






Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs 


Ikiwa ni kipindi Cha maadhimisho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Chakula cha pamoja na watoto yatima na waishio katika mazingira  magumu wapatao 300 pamoja na wajane 100 wanaohudumiwa na kufadhiliwa na shirika la Tumaini foundation Jijini Hapa. 

Hafla hiyo imefanyika Disemba 26 katika ukumbi wa Lavana uliopo Ihumwa Jijini Dodoma. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhe. Senyamule amempongeza Mkurugenzi wa Shirika hilo Ndg. Tumaini Kivuyo kwa Moyo wa huruma wa kuwasaidia na kuyahudumia Makundi maalum kwani shirika hilo linalenga kuwahudumia watoto yatima, watoto wanaofanya kazi mitaani kabla ya umri wao wa kujitegemea pamoja wajane ambao hupatiwa huduma za Elimu, Ujasiriamali, Matibabu pamoja na kuwawezesha kiuchumi.

Aidha Mhe. Senyamule ametumia wasaa huo kukemea vikali tukio la mauaji ya mtoto wa miaka 6 lililotokea Disemba 25, 2024 Kata ya Ilazo Jijini Dodoma ambapo amewaasa wanajamii kuhakikisha wanakuwa walinzi wazuri wa watoto kwa kuhakikisha wanakuwa salama na kuweka bayana kuwa yeyote atayebainika kufanya ukatili atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule ametoa maelekezo kuwa wanufaika Watoto na Wajane waliosaidiwa watumie vizuri fursa ya msaada katika kujiendeleza ili waweze kujitegemea,  wazazi na Walezi kuhakiksha wanatekeleza wajibu wao wa kuwatunza na kuwalinda Watoto wakati wote, ⁠Jamii kutambua Kaya zilizopo katika mazingira hatarishi na kuzisaidia.

Watendaji wa Serikali kuendelea kutambua Kaya zilizopo katika mazingira hatarishi kwa kuziunganisha na fursa za Mikopo ya Serikali Kupitia Halmashauri pia kuendelea Kutoa Elimu Juu ya manufaa ya 30% kwa wazee, Wanawake, Vijana na Watu Wenye ulemavu Kupitia Sheria ya Manunuzi na fursa mbalimbali zilizopo Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na  kuhuisha  Kamati za kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ngazi zote za Halmashauri.




 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA