RC SENYAMULE ATAKA HATUA KALI ZICHUKULIWE DHIDI YA WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA SERIKALI


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule akitoa maagizo wakati wa kufunga kikao hicho hapo jana Disemba 18, 2024 ambapo alitaka Wakuu wa Wilaya kuja na Mkakati wa kuzuia wizi wa miundombinu ya Serikali.





Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akiwakumbusha wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma majukumu ya kikao hicho kabla ya kuanza kikao hapo jana katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma





Wakuu wa Wilaya za Kondoa na Mpwapwa (wa kwanza na pili kushoto) wakiwa na Makatibu Tawala wa Wilaya za Bahi na Dodoma Mjini ambao wote ni wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa kikao hicho.





Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wakifuatilia maagizo ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa kikao cha kwanza kwa mwaka 2024 / 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Dodoma




Na. Hellen M. Minja,
       Habari – DODOMA RS


Kufuatia wimbi la wizi wa vifaa vya miundombinu ya Taasisi za Serikali, agizo limetolewa kwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma kukaa na kupanga mkakati wa namna ya kukabiliana na changamoto hiyo inayowagharimu wananchi kwa kukosa huduma za msingi, lakini pia kuitia Serikali hasara kubwa.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa kikao cha kwanza kwa mwaka 2024/2025 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma kilichofanyika Disemba 18, 2024 katika ukumbi wa ofisi yake Jijini Dodoma.

“Suala la wizi wa miundombinu linasikitisha sana, si kiashiria kizuri kuendelea kukifumbia macho na tupeane majukumu, wakuu wa Wilaya  nendeni katika Wilaya zenu mkakae, mje na mikakati ya namna gani mnakwenda kukabiliana na wizi wa miundombinu ya Serikali na ninawapa muda, mpaka mwishoni mwa mwezi Desemba ” Mhe. Senyamule.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa kushirikisha Wananchi kwenye miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kila mmoja  awe sehemu ya miradi hiyo kwani wao ndio wanufaika na walinzi pia.

“Kuna utaratibu ambao upo kwenye miradi ya Serikali unaosema, kila mradi unapokwenda kwenye Kijiji, Kata, ni lazima wananchi washirikishwe kwenye mradi husika, lazima taarifa ibandikwe kwenye Serikali ya kijiji, ofisi au Kata ili kila mwanakijiji ajue na awe sehemu ya mradi” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Akizungumzia hali ya Barabara za Mkoa hasa kipindi hiki cha mvua, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS, Mhandisi Zuhura H. Amani amesema;

“Sehemu kubwa ya mtandao wa barabara za Mkoa ziko katika hali nzuri,isipokua baadhi ya barabara ambazo ziliharibiwa na mvua hali iliyosababisha baadhi ya maeneo kutopitika ,na mengine kupitika kwa shida. Hadi kufikia mwishoni mwa Novemba, 2024, matengenezo ya kuimarisha au kurudisha mawasiliano yamefanyika na mengine yanaendelea” Mhandisi Zuhura.

Katika wasilisho la Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA),pamoja na mambo mengine, lilizungumzia mapitio ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo kwenye utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya matengenezo ya barabara zimetenga jumla ya shilingi 36,152,430,180.00 kati ya fedha hizi, shilingi 34,545,682,494.00 ni kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa miundombinu ya barabara na 1,606,747,686.00 kwa ajili ya shughuli za utawala, usimamizi, ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya miundombinu ya barabara ngazi ya Mkoa na Wilaya.

Awali, katibu tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya alikumbusha kuwa vikao vya bodi ya barabara ambavyo hufanyika mara mbili kwa mwaka ni kwa mujibu wa sheria na moja ya jukumu la bodi hiyo ni kushauri na kutoa mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ya barabara kuhusiana na ujenzi au uendelezaji wa mtandao wa barabara katika Mkoa husika  

 

 

#dodomafahariyawatanzania 
#keroyakowajibuwangu 
 #mtiwangubirthdayyangu








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA