RC SENYAMULE AZIAGIZA HALMASHAURI ZA DODOMA KUUNDA KAMATI ZA ULINZI NGAZI YA KATA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Dodoma.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) , Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe (kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Injinia Happiness Mgalula wakiwa katika kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa Hlmashauri ya Jiji  ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba.



Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo akiainisha sababu zinazochangia uwepo wa watoto wa mtaani na ombaomba katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kujadili namna ya kukabiliana na changamoto ya watoto wa mtaani Jijini humu.


 



Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma wakisikiliza kwa makini maagizo yaliyotolewa na Mhe. Senyamule wakati kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Dodoma.




Baadi ya wajumbe na wadau waliohudhuria kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Dodoma.





Na; Siza Kangalawe 
      Habari - Dodoma RS 

Mkuu wa mkoa wa dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amewataka wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Dodoma kuanzisha kamati za ulinzi ngazi ya kata na mitaa ili kubaini watoto wanaotumikishwa na wazazi kama kitega uchumi.

Agizo hilo limetolewa  Disemba 21,2024 wakati wa kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi za mitaani kilichofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji Mtumba Jijini hapo.

“ Naziagiza Halmashauri  zote kuanzisha kamati za ulinzi na usalama za Kata na Mitaa ili kubaini watoto wanaotumikishwa na wazazi kama kitega uchumi", Ameagiza Mhe. Senyamule 

Sambamba na hilo Mhe. Senyamule amehimiza kila Halmashauri  kuweka sheria ndogondogo zitakazo saidia kutoa adhabu kwa wazazi/walezi  wanaowatumikisha watoto kwenye kazi za mtaani.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Mwaipopo ameainisha sababu zinazochangia uwepo wa watoto wa mtaani na ombaomba katika Mkoa huu zikiwemo hali ya kukua kwa Mkoa na Miji , kuwepo kwa migogoro katika ndoa, hali ya uyatima, ukatili ndani ya familia , umasikini na kukosekana kwa sheria ndogo ndogo katika Halmashauri zinazowajibisha jamii, wazazi na walezi wasiozingatia usimamizi wa haki za watoto na watu wenye ulemavu wanaotumikishwa. 

Kwa upande wake Mfanyakazi kutoka Shirika la SOS Children’s Villages Bw. Damas Damas Amedeus amesema mbali na changamoto hizo wamekuwa wadau muhimu wa masuala ya watoto katika kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wanatimiza haki zao za msingi  na kukabiliana na kadhia wanazozipata.



#dodomafahariyawatanzania








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA