SERIKALI YAKABIDHIWA KITUO CHA AFYA ILAZO.





















Na Sofia Remmi 
Habari-Dodoma Rs.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Makabidhiano ya  Kituo cha afya  Ilazo  kilichojengwa Kwa ufadhili wa shirika la 'Korea International Cooperation Agency' ( KOICA) kwa kushirikiana na ' The United Nations Children's Fund ' ( UNICEF ). 

Mashirika hayo yameikabidhi Serikali ya Mkoa kituo tayari kwa matumizi ya kuwahudumia Wananchi wa kata ya  Ilazo na maeneo jirani. 

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Senyamule amesema majengo hayo ya huduma za afya yamejengwa na kufadhiliwa na Shirika la la Korea KOICA Kupitia UNICEF.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana lengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga kwa kuleta huduma bora kwa wananchi wake kila kijiji na kila  mtaa.

“Uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto imewezeshwa kwa kiasi kikubwa kwa kujenga vituo vya kutolea hiduma za afya, ununuzi wa dawa na  vifaa tiba kwenye kila halmashauri na kuwezesha Mkoa na kupokea kiasi cha shilingi Bilioni 34.51 kwa mwaka wa fedha 2022/23 na 2023/24 kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya huduma za afya na kiasi cha shilingi Billioni 34.20 kwaajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, Mashine,” amesema Senyamule.

Kupitia fedha hizo zimejenga hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Chemba, Chamwino, Kondoa na Dodoma Mjini, na kuweka mahusino mazuri baina ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Korea.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dkt.Pima Sebastian amesema lengo la Mradi huu ni kuboresha huduma za Afya ya mama na Mtoto na huduma za upasuaji,  Mradi huu umeanza kutelelezwa mnamo tarehe 04/07/2023 na Ulikamilika 30/09/204.

“Mradi huu ulianza kutoa huduma tarehe 01/10/2024 na kupokea wateja/ wagonjwa  479 waliohudumiwa wakiwemo kina mama wajawazito na watoto chini ya Miaka mitano 212 na wagonjwa wa nje 267. kituo kina jumla ya watoa huduma 24 wakiwemo madaktari 05, wauguzi 10, wateknolojia maabara 02, wateknolojia dawa 02, wataalam watoa dawa za usingizi na gazi salama 02, tabibu meno 01, Katibu afya na Afisa lishe 01”

Hata hivyo Dkt. Sebastian amesema kituo hicho kimetumia  jumla ya shilingi Bilioni 3.2 hadi kukamilika kwake  kwaajili ya ujenzi na ununuzi wa vifaa tiba.














 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA