"WANANCHI TOENI TAARIFA JUU YA VITENDO VYA UKATILI" -RC SENYAMULE.
Na Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameyasema hayo leo tarehe 23 Disemba 2024 katika kikao cha Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza ukatili dhidi wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Akizungumza na wajumbe wa kamati iyo Rc Senyamule amesema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili vinavtofanyika mahali popote walipo.
Ameongeza kuwa, kamati ya Ulinzi wa wanawake na watoto Mkoa wa Dodoma, imeanzisha mpango kazi huo ili kupunguza na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaume.
“Ukatili husababisha athari nyingi ikiwemo mimba za utotoni, ulemavu na kuambukizwa VVU na UKIMWI. Serikali ya awamu ya sita imejipanga thabiti kupambana na ukatili wa aina yoyote unaotokea Katika Jamii.
“Pia, vitendo vya ukatili husababisha kutoshiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kuigharimu Serikali fedha nyingi katika shughulikia vitendo vya ukatili” Mhe. Senyamule.
Pamoja na juhudi mbalimbali za kutoa elimi kwa Jamii dhidi ya vitendo vya ukatili, Mkoa umejipanga na unaendelea kukabiliana na ukatili wa Kingono, kihisiaBna aina nyingine za ukatili.
Vile vile, Afisa ustawi wa Jamii wa Mkoa Bi. Josephine Mwaipopo ameyataja malengo ya mpango kazi wa awamu ya pili ya MTAKUWWA.
“Malengo ya MTAKUWWA ni kusimamia utekelezaji wa afua za kuzuia ukatili na kutoa msaada, utelezaji na kusimamia sheria, kuwezesha Mazingira salama katika maeneo ya umma, kuimarisha uchumi wa Kaya na kupunguza ukatili, pamoja Serikali kuzuia ukatili ndani ya jamii” Amesema Mwaipopo.
Comments
Post a Comment