DODOMA WAPANDA MITI 1,480 KUADHIMISHA BIRTHDAY YA MHE. RAIS
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumzia umuhimu wa kupanda miti baada ya kukamilika kwa zoezi hilo lililoashiria hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akiotesha mti kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya birthday yangu mti wangu wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akiotesha mti kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya birthday yangu mti wangu wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Fatma Toufiq akiotesha mti kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya birthday yangu mti wangu wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Meneja wa Kanda ya Kati Benki ya NMB Bi. Janeth Shango akiotesha mti kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya birthday yangu mti wangu wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Baadhi ya miche ya miti iliyooteshwa wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025 ambapo miti 1,480.
Kikundi chaWanawake na Samia Mkoa wa Dodoma ambacho kilishiriki kwenye kampeni ya birthday yangu mti wangu wakiwa wamebeba miche ya miti tayari kwenda kuiotesha kwenye eneo lililoandaliwa wakati wa hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguzi Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muunga o wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 27, 2025, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Taasisi na vikundi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huu Mhe. Rosemary Senyamule, wamepanda miti 1,480 katika eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na ukataji keki pamoja na shampeni, Mhe. Senyamule amemtaja Mhe. Dkt Samia kama muasisi wa kampeni ya kukijanisha Dodoma.
“Mhe. Dkt. Samia ndiye alianzisha kazi ya kukijanisha Dodoma alipozindua upandaji miti na neno la ‘Dodoma ya Kijani’ lilianza wakati huo akiwa Makamu wa Rais mwaka 2017 pale Mzakwe ambapo alipanda miti. Tangu wakati huo, tuliendelea na kauli mbiu ya kusema Dodoma ya Kijani na yeye akisema dhamira yake ya kutamani Dodoma kuwa ya kijani”
Aidha, amehimiza kufuatwa kwa sheria zilizowekwa juu ya upandaji miti kwa mtu mmoja mmoja miti mitano na Taasisi miti 20;
“Leo tumejikumbusha kupitia siku ya kuzaliwa Mhe. Rais ambaye kwa umoja wetu tumeona thamani ya kukutana hapa. Jiji na Halmashauri, tusimamie sheria hizi kwa sababu miti ni uhai ili baadae, kila mtu ajivunie kuwa sehemu ya kubadilisha mazingira ya Dodoma” Mhe. Senyamule.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, amesema, kati ya miti iliyopandwa siku ya leo, miti 20 ni ya tiba asili ambapo chama cha tiba asili kimefika Mkoa wa Dodoma kuunga mkono juhudi za kutunza mazingira na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani ili kufanana na Makao Makuu ya nchi.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri amesema kumekua na mwitikio mkubwa kwa wakazi wa Dodoma kwenye zoezi la upandaji miti huku akitoa rai kwa kila mmoja kupanda miti wakati wa kumbukizi yake ya kuzaliwa kwani kwa kufanya hivyo, ajenda ya kukijanisha Dodoma itafanikiwa kwa haraka zaidi.
#dodomafahariyawatanzania
#27yamamamtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment