HUDUMA ZA KISHERIA ZATOLEWA DODOMA KUELEKEA FEBRUARI PILI
Mtoa huduma za Kisheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rose Mtani akimuelekeza mwananchi kuweka sahihi kwenye kitabu cha wageni pindi alipotembelea Banda la Sheria la Mkoa linalopatikana kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma likitoa huduma kuelekea maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria Februari 02, 2025.
Mtoa huduma za Kisheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Rose Mtani, akimsikiliza mwananchi aliyetembelea Banda la Sheria la Mkoa linalopatikana kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma juu ya changamoto yake inayohitaji msaada wa kisheria kuelekea maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria Februari 02, 2025.
Na. Sizah Kangalawe Habari- Dodoma Rs
Ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini yanayofanyika katika viwanja vya 'Nyerere Square' Jijini Dodoma, Banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kupitia kitengo Cha Sheria linapatikana katika viwanja hivyo.
Huduma mbalimbali za kisheria zinatolewa katika banda hilo pasi na gharama yoyote.
Wananchi na wakazi wote wa Dodoma mnakaribishwa kutembelea maonesho hayo yanayotarajiwa kufikia kilele Februari 2/2025 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini hapa, na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Comments
Post a Comment