KLABU YA MAZINGIRA PALACE SCHOOL YAMTEMBELEA RC SENYAMULE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na wanafunzi wa Klabu ya Mazingira kutoka shule ya msingi Palace ya Jijini Dar Es Salaam (hawapo pichani) walipofika ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025 kwa lengo la kumpongeza kwa jitihada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti, hususan kwenye kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais wa Tanzania.
Mkuu wa shule ya Palace ya Jijini Dar Es Salaam Mwalimu Ferdinand E. Ilungu, akielezea lengo la ujio wa Klabu ya Mazingira ya shule yake kwenye Mkoa wa Dodoma ambalo ni kuunga mkono jitihada za kulinda mazingira kwa kupanda miti pindi walipomtembelea Mkuu wa Mkoa huu Ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025
Klabu ya Mazingira kutoka shule ya msingi Palace ya Jijini Dodoma walipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Jengo la Mkapa Jijini Dodoma ili kumpongeza kwa jitihada za kutunza mazingira kupitia kampeni mbalimbali za kupanda miti hususan siku ya leo Januari 27, 2025 wakati wa kumbukizi ya kuzaliwa Rais wa Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Klabu ya Mazingira kutoka shule ya msingi Palace ya Jijini Dar Es Salaam walipofika ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Januari 27, 2025 kwa lengo la kumpongeza kwa jitihada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti, hususan kwenye kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais wa Tanzania.
Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Wanafunzi wa klabu ya mazingira kutoka shule ya msingi Palace ya Jijini Dar es Salaam, leo Januari 27, 2025, wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ofisini kwake Jengo la Mkapa JIjini Dodoma kwa lengo la kumpongeza kwa jitihada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti, hususan kwenye kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais wa Tanzania.
Mhe. Senyamule amewaelezea wanafunzi hao dhamira ya Mkoa wa Dodoma kuenzi kampeni ya kupanda miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pia kufuta historia ya ukame iliyokua katika Mkoa huu kwa miaka mingi.
“Mabadiliko ya tabia nchi yanatutaka tuhakikishe tunarudisha uoto wa asili na hali ya hewa nzuri ili maisha mazuri yaendelee. Tunao wajibu wa kurekebisha mabadiliko ya tabia nchi lakini kubwa ni suala la kupanda miti, na nyinyi mmekuja na ajenda hiyo hiyo. Tunaamini baada ya muda mfupi, Dodoma itakua tu na historia ya ukame”
Wanafunzi hao wakiongozwa na Mkuu wa shule Mwalimu Ferdinand E. Ilungu, wamefika ofisini hapo kuunga mkono jitihada hizo kwani wamekua wakifanya kazi ambayo Mhe. Rais ameipa kipaumbele.
“Tunafanya kazi ambayo Mhe. Rais amekua akiipa kipaumbele hususan kupitia watoto kwenye suala zima la utunzaji mazingira. Watoto hawa kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameshafanya kazi ya kupanda miti zaidi ya 4,000. Katika siku maalumu ya Mhe. Rais, tumeona ni vema tukakutembelea kwa maana ya kutambua kazi yako na kukupa pongezi” Amesema Mwl. Ilungu
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment