MKURUGENZI MKUU MPYA TAKUKURU AJITAMBULISHA MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw. Fransic Chalamila aliyeteuliwa hivi karibuni alipomtembelea ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma.





Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Victor Swella (aliyesimama), awali akimtambulisha Mkurugenzi mpya wa Taasisi hiyo Bw. Fransic Chalamila alipokwenda kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Makao Makuu ya nchi.






Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa TAKUKURU Mkoa akiwemo Mkurugenzi Mkuu Bw. Fransic Chalamila alipofika ofisini kwake kujitambulisha hii leo.






Na. Hellen M. Minja,
       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, leo Januari 08, 2025, ametembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw. Fransic Chalamila aliyeteuliwa hivi karibuni, lengo likiwa ni kujitambulisha kwenye ofisi ya Mkoa na Makao Makuu ya Nchi.

Mhe. Senyamule ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi huyo kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo huku akimtaka kuusaidia Mkoa kwenye usimamizi wa miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani ya Makao Makuu kwani bado inaendelea kujengeka.

Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, ameshukuru ushirikiano wa Taasisi hiyo na Serikali ya Mkoa hasa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani Mhe. Rais ametoa fedha nyingi kwayo, hivyo Mkoa una dhamana ya kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa.

 Mkurugenzi huyo ametoa shukrani kwa Serikali ya Mkoa kwa ushirikiano unaoipatia Taasisi yake na kusema kuwa Taasisi ina majukumu mengi zaidi ya kushughulikia rushwa ikiwemo kufuatilia utekelezaji wa miradi na upatikanaji wa huduma kwa jamii ili wananchi wafurahie na kuendelea kuiamini na kuipenda Serikali yao.

Mkurugenzi Mkuu huyo  aliambatana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Victor Swella pamoja na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Euginius Hazinamwisho


#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu                              
#mtiwangubirthdayyangu





 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA

KAMATI YA USALAMA MKOA WA DODOMA YAFANYA ZIARA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO, KONDOA