RC SENYAMULE AZINDUA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na Wajumbe wa Bodi mpya ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma sambamba na wadau wengine wakiwemo Watumishi wa Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali Jijini Dodoma leo Januari 29, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizindua rasmi Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali hiyo Jijini Dodoma leo Januari 29, 2025.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali Jijini Dodoma leo Januari 29, 2025.
Picha juu na chini, baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na Wajumbe wa Bodi mpya ya Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali Jijini Dodoma leo Januari 29, 2025.
Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) imepata Bodi mpya ya ushauri itakayofanya kazi kwa karibu na Uongozi wa Taasisi hiyo ambayo imezinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali hiyo Jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Senyamule amesema, ana Imani na bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Ezekiel Mpuya kwamba itakwenda kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Hospitali hiyo.
“Nina imani na bodi hii. Ina mambo mengi lakini, ina uwezo mkubwa wa kufanya ushawishi huko kwenye Wizara husika tukaweza kufanya mabadiliko makubwa kupitia hospitali hii. Umuhimu wa kuboresha rufaa hii ni mkubwa kwani hatuhudumii tu wakazi wa Dodoma bali watu wengi kutoka Mataifa mbalimbali,” Mhe. Senyamule.
Kadhalika, Mganga Mfawidhi wa Hospitali na Katibu wa Bodi hiyo Dr. Ernest Ibenzi, amesema, Hospitali yake sasa inajipambanua kwa huduma bora za mifupa na inatarajia kuanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
“Tunatarajia kuanzisha kitengo maalumu cha huduma za mifupa hapa kitakachojulikana kama DOI yaani ‘Dodoma Orthopaedic Institute’ kama ilivyo MOI pale Muhimbili kwa kua huduma za kibingwa kwa wagonjwa wa mivunjiko na mifupa zinazotambulika Kimataifa, zinafanyika hapa. Hospitali imewezesha upatikanaji wa vifaa tiba na uanzishwaji wa huduma za upasuaji mifupa katika hospitali za rufaa za Mikoa ya Arusha, Geita, Njombe, Bukoba, Shinyanga, Mwananyamala, Iringa, Tumbi, na Morogoro lengo ni kuzifikia hospitali zote za Mikoa ambazo hazina huduma hii,” Dkt. Ibenzi
Hata hivyo, akitoa shukrani zake kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi, Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa Mjumbe wa Kamati kuu umeipa uzito Bodi hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kuwa itaweza kufanya kazi kwa urahisi na kuwafikia watoa maamuzi kwa haraka na kuahidi kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment