WAZIRI MKUU WA UGANDA AZURU KIWANDA CHA ITRACOM DODOMA.




Picha juu na chini, Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja (wa pili kulia) akisalimiana na wenyeji wake alipowasili kwenye kituo cha Treni ya kisasa ya SGR Mkonze Jijini Dodoma, pindi alipofika Mkoani hapa kwa ajili ya kufanya ziara ya siku moja kwenye kiwanda cha mbolea cha Itracom kilichopo Kata ya Nala Jijini Dodoma jana Januari 29, 2025.






Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja (katikati) akiwa na wenyeji wake Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (wa kwanza kulia) pamoja na viongozi wa kiwanda cha mbolea Itracom Jijini Dodoma, wakati  alipotembelea kiwanda hicho Januari 29, 2025 kujionea namna uzalishaji wa mbolea ya kisasa unavyofanyika.







Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja (katikati) akiwa na wenyeji wake Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (wa kwanza kulia, mbele), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kulia) kwenye moja ya chumba cha kuhifadhia mbolea iliyokwishachakatwa tayari kwa matumizi katika Kiwanda cha mbolea Itracom Jijini Dodoma




.

Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja, akizungumza na wenyeji wake pamoja na viongozi wa kiwanda cha mbolea cha Itracom (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutamatika kwa ziara yake katika kiwanda hicho.




 


Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo, akizungumzia namna ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda unavyochagiza ukuaji uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutamatika kwa ziara ya Waziri Mkuu wa Uganda kwenye kiwanda cha mbolea Itracom.







Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimuelezea Waziri Mkuu wa Uganda namna ambavyo nchi yake inaweza kunufaika na mbolea inayozalishwa na kiwanda cha Itracom kwakua inasambazwa nchi zote za Afrika Mashariki, wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutamatika kwa ziara ya Waziri Mkuu huyo kiwandani hapo.







Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha mbolea Itracom Bw. Nduwimana Nazaire akitoa taarifa na historia ya kiwanda chake mbele ya Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma, baada ya kutamatika kwa ziara ya Kiongozi huyo katika kiwanda hicho Januari 29, 2025








Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja, (katikati) akifuatilia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa kwake wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutamatika kwa ziara yake katika kiwanda cha mbolea Itaracom kilichopo Kata ya Nala Januari 29, 2025.





Baadhi ya watumishi wa Kiwanda cha mbolea Itracom, wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana, iliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutamatika kwa ziara ya Kiongozi huyo katika kiwanda chao kilichopo Kata ya Nala Januari 29, 2025.






Na. Hellen M. Minja, 
       Habari – DODOMA RS

Nchi ya Tanzania imetajwa kuwa na ardhi nzuri kwa kilimo na kwa kutumia teknolojia za kisasa, inaweza kuzalisha chakula cha kutosha kulisha Afrika nzima. Hayo yamebainishwa Januari 29, 2025 na Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Robinah Nabbanja, alipofanya ziara ya siku moja kutembelea kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Itracom kilichopo Nala Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika kwenye Hoteli ya Morena Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea kiwanda hicho na kujionea namna uzalishaji wa mbolea kwa ajili ya kilimo unavyofanyika.

“Uganda na Tanzania zina bahati ambayo nadhani imetolewa kimkakati na Mwenyezi Mungu na ni lazima tuilishe Dunia. Nimetembelea nchi za kiarabu, watu wake hawana ardhi lakini wanapaswa kuishi. Wana teknolojia ambayo sisi hatuna hivyo, kama tukizalisha vya kutosha, tutalisha nchi za kiarabu,” Mhe. Nabbanja 

Waziri Mkuu huyo ameongeza kuwa, Uganda na Tanzania zinatakiwa kufikiria namna zinavyoweza kuboresha uchumi ambao unawezekana kupitia kilimo kwani soko la Uganda limejaa bidhaa za kilimo na ufugaji kutoka Tanzania kwa kuwa sasa zinapitishwa bila kodi hivyo ni wakati muafaka wa kuangalia fursa za masoko ya nje.

Nae, Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe. Selemani Jafo amesema ugeni huo unaweka alama ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili ambapo urafiki huo unachangia kukuza maendeleo ndani ya umoja wa nchi za Afrika Mashariki na nyingine. Ameongeza kuwa, uzalishaji wa mbolea bora unahakikisha usalama wa chakula, unakukuza kilimo na uchumi kwa ujumla.

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amempongeza kiongozi huyo kwa kutembelea Dodoma na kusema; 

“Uganda inaweza kunufaika na mbolea inayotengenezwa katika kiwanda cha Itracom kwani kinafanya usambazaji kwenye nchi zote za Afrika Mashariki na pia kuna fursa ya kujifunza matumizi ya mbolea kupitia mashamba darasa yanayopatikana hapa ambayo yanafanya vizuri”. Mhe. Senyamule 
  


#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu






















 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA