PBZ WAMTEMBELEA KATIBU TAWALA MKOA WA DODOMA
Na.Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs
Uongozi wa Bank ya PBZ umemtembelea Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma,mapema Februari 19,2025.
Lengo la ziara hiyo ni kusalimia na kuzungumza kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Dodoma.
Uongozi huo uliambatana na Meneja wa Benki ya PBZ Dodoma Bi. Mwanaharusi Ally na Afisa Mahusiano Abdul Khamis.
#dodomafahariyawatanzania.
#keroyakowajibuwangu.
Comments
Post a Comment