DODOMA YAPO MADINI YA KUTOSHA"-RC SENYAMULE.

 













Na Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kiwanda cha Kuchenjua Mawe ya Shaba kwenda Kwenye Shaba halisi.

Ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 16 Februari 2025 katika Mtaa wa Nala, Kata ya Nala, iliandaliwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Mhe. Senyamule Amesema tunaendelea kufurahi kuona mambo mazuri yanayoendelea kutokea katika Mkoa wetu kwa kuongezeka kiwanda ambacho vijana wengi watanufaika nacho.

“Hii ni moja ya fursa ambayo vijana wengi watanufaika nayo kwa kupata ajira katika kiwanda hiki hivyo niendelee kupongeza Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu hodari Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan”

“Madini ni kitu cha Mkakati Katika Mkoa wetu na yanazidi kuongezeka kwa wingi zaidi na Kuzidi kuifaharisha dodoma kwa kuwajali wawekezaji ambao wanaendelea Kuja na tunazidi kuwapokea maana bado Mkoa una madini Mengi na unahitaji wawekezaji wa viwanda kama hawa wa kampuni ya Shengde precious Metal LTD” Amesema Senyamule.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Abia Mosses Mafie amesema kuongeza thamani ya madini kwa kuzalisha copper cathode ulianza rasmi tarehe 28 Novemba 2024. Tangu kuanza kwake, Mradi umefanikiwa hatua kadhaa muhimu hadi kufikia tarehe 15 Februari 2025, ndani ya kipindi cha siku 80. 

Tangu kuanza kwa mradi huu, jumla ya shilingi milioni 160 za Kitanzania zimetumika. Bajeti inayokadiriwa kwa mradi mzima ni Dola za Kimarekani milioni 1.2. ambayo ni sawa na Bilioni 3.



#dodomafahariyawatanzania 
#keroyakowajibuwangu.












Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA