Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wa matunda katika shule ya Sekondari Kisasa ya Jijini Dodoma kwa lengo la kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni za Uchumi na Mazingira kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Aziza Mumba akipanda mti wa matunda katika shule ya Sekondari Kisasa ya Jijini Dodoma kwa lengo la kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akimwagilia mti uliopandwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisasa Jijini Dodoma kwa lengo la kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Moja kati ya miti 140 ya Matunda iliyopandwa kwenye shule ya Sekondari Kisasa ya Jijini Dodoma kwa lengo la kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea risala ya wanafunzi kutoka kwa mwakilishi wao baada ya zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule ya Sekondari Kisasa ya Jijini Dodoma lililolenga kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi mti wa matunda kwa Mwalimu wa shule ya Sekondari Kisasa ya Jijini Dodoma wakati wa zoezi la upandaji miti katika shule hiyo lililolenga kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisasa wakimsikiliza Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule hiyo ya Jijini Dodoma lililolenga kukijanisha Dodoma na kuenzi siku ya Wapendanao leo Februari 14, 2025
Na:Sofia Remmi,
Habari-Dodoma Rs
Ikiwa ni muendelezo wa jitihada mahususi za kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa Kijani,leo Februari 14,2025 ,ambapo ni Siku ya Wapendanao, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa Mazingira, wamepanda miti ya matunda katika shule ya Sekondari Kisasa,kama namna mojawapo ya kusheherekea siku hiyo.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu Bw.Vicenti Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma,amesema kila mwanafunzi ana wajibu wa kusimamia miti hiyo ili kuhakikisha inakuwa vizuri.
Akizungumza na wadau waliojitokeza Bw.Kayombo amesema miti 140 iliyopandwa leo itunzwe vizuri ili kutimiza lengo na adhma ya Viongozi wa Mkoa kukijanisha Dodoma.
“Wanafunzi waliopendekezwa kutunza miti hii niwasihi tunzeni miti hii kwani ina faida nyingi,mkizingatia kuwa ni miti ya matunda ,itawasaidia wanafunzi wote hapa mlipo.
Kupitia miti hii mtapata matunda,itunzeni huku mkizingatia pia kuwa Mkuu wa Mkoa wetu ni kinara namba moja wa Utunzaji Mazingira.Miti hiii ikitunzwa vizuri wanafunzi wote mtafaidika na matunda yake” amesema Kayombo.
Kwa upande wake Kiongozi wa wanafunzi katika Shule hiyo, amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali hata kuwaletea miradi ya ujenzi wa madarasa ambayo yamewezesha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kusomea na kuahidi kuisimamia miti hiyo ili iweze kukua vizuri.
Tukio hilo la upandaji wa miti limewezeshwa na taasisi ya Go-Plant-Tanzania ambayo ilitoa Miche ya miti ya matunda 140, kaulimbiu ikiwa ni “HUBA LANGU, MAZINGIRA YANGU”
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#kijanishadodoma
#hubalangumazingira yangu.
Comments
Post a Comment