KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO MAANA YAKE TULENGE VIFO SIFURI : RAS MMUYA
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya Februari 24/ 2025, ametembelea Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kufanya ufuatiliaji akilenga huduma ya Mama na Mtoto.
Katika ziara hiyo Bw. Mmuya aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Thomas Rutachunzibwa pamoja na watendaji wengine kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Akizungumza akiwa hospitalini hapo Mmuya amesema "Sisi tuna jukumu la kulinda Afya ya Mama na Mtoto,maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa watendaji wake ni nendeni mkasimamie eneo hili.Yeye Mhe. Rais amewekeza vya kutosha kuzuia vifo vya Mama na Mtoto,sisi hatumdai, lakini yeye anatudai sisi.Mmeapa kuokoa maisha ya watu,hakikisheni mnafanya hivyo.
Kuokoa maisha ya Mama na Mtoto,maana yake tulenge 'zero death'.Tuendelee kufanya kazi kwa bidii,kwa kujiamini,lengo letu likiwa ni kuona watu wanaendelea kubaki na uhai wao.Kila mtu afanye kazi yake,hata ifike mahali moyo wako useme,nilifanya 'to the best' ".
Aidha Daktari Rutachunzibwa,amemshukuru Katibu Tawala kwa kufika na kufanya ufuatiliaji huo,huku akitoa angalizo kwa watumishi wa Hospitali hiyo kwamba ziara ya Katibu tawala katika hospitali hiyo ni ishara kuwa wanafanya kazi na Viongozi makini,na kwamba Serikali imedhamiria kupambana na vifo vinavyotokana na uzazi.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#karibudodoma
Comments
Post a Comment