RAS MMUYA ATOA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MAGUO.

 












Na Sofia Remmi.
Habari-Dodoma Rs

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar K.Mmuya ametoa salamu za Pole kwa Familia na waombolezaji mbalimbali kufuatia kifo cha Mhe. Abdallah Maguo aliyekuwa Diwani na Mwenyekiti na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, aliyefariki tarehe 24 Februari 2025,katika hospitali ya Benjamin Mkapa wakati akipatiwa matibabu.

RAS Mmuya amewaombea faraja ya mwenyezi Mungu iwafikie familia,ndugu,jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.

Akizungumza na waombolezaji RAS  Mmuya amesema marehemu Maguo alikuwa muadilifu aliyezingatia maadili ya kazi yake ya kuwatumikia wananchi wake wa Kata ya  Mnenia wakati wote.

“ Jambo la msiba si jambo la kuzoeleka, na njia pekee ya Kumuenzi Maguo ni kuyaenzi mema yake ya wakati wote kipindi cha uhai wake.

Muda wa kuishi duniani ni mfupi sana tunapaswa kutenda mema wakati wote sio kwa ajili yetu,bali kwa ajili ya wote” Amesema Mmuya. 

Aidha msiba huo umefanyika Katika Kijiji cha Mnenia kata ya Mnenia Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa  tarehe 25 Februari 2025. Marehemu Abdallah Maguo  ameacha Mjane Mmoja, watoto watatu na wajukuu Saba .Wote ni wa  Mwenyezi Mungu,na kwake tutarejea.

#dodomafahariyawatanzania 
#keroyakowajibwangu












Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA