RC SENYAMULE ATOA MAELEKEZO KWA TRC DODOMA SUALA LA FOLENI

 












Na; Happiness E. Chindiye 
       Habari - Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule leo  Februari 17,2025 ametembelea Stesheni ya SGR  ya Samia Suluhu Hassan iliyopo Mkonze  Jijini Dodoma kujionea namna huduma zinavyotolewa, hususani wakati wa kushuka abiria.

Lengo la ziara hiyo ni kutatua changamoto zilizoibuliwa na abiria wanaoshuka eneo hilo na kukumbana na adha ya foleni inayotokana na uwepo wa mageti machache ya kuhakiki stakabadhi za malipo ya ushuru wa vyombo vya moto vinavyotoka katika Stesheni hiyo.

Akizungumza na Uongozi wa TRC Dodoma, baada ya abiria kushuka majira ya saa 07;25 na kujionea hali halisi,Mhe. Senyamule ametoa maelekezo haya

 “Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan, ameleta SGR, ni jambo zuri sana lakini sasa tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa Stesheni hii kuhusu kero ya msongamano wa magari unaosababishwa na idadi ndogo ya mashine za kusoma tikeketi za magari wakati wa kutoka.

Naagiza mashine hizi za kuscan magari wakati wa kutoka ziongezeke, lakini pia geti la kutoka litenganishwe kati ya magari na pikipiki ili kupunguza msongamano huu kwani hali hii haipendezi kwenye usafiri huu wa kisasa,”Amesema Mhe. Senyamule

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema maagizo hayo yafanyiwe kazi ndani ya wiki moja ili kuwaondolea adha watumiaji wa usafiri huo Nchini.

“Nipate taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya, wasilianeni na TRC Makao Makuu ili kuona ni kwa namna gani mnaweza kulimaliza suala hili ndani ya wiki moja isifike mwezi mmoja, watu wanapanda treni hii kuokoa muda lakini nyie mnawachelewesha hapa na wengine wana wagonjwa.

Nikiwa hapa hapa nimeshuhudia tumesimama zaidi ya dakika 41 ndiyo gari la mwisho linapita kwenye mashine, sasa kama mimi nipo hapa gari zimetumia muda huo, inakuaje mnapokuwa wenyewe si muda unakwenda zaidi ya huo,”Amesema Mhe. Senyamule

Usafiri wa treni za Umeme  ulizinduliwa rasmi Agosti 1, mwaka 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan, na kushuhudiwa na Viongozi wengine wakuu wa Nchi.




#dodomafahariyawatanzania 
#keroyakowajibuwangu 
#birthdayyangumtiwangu








Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA