RS DODOMA NA UTAMADUNI WA CHAKULA CHA PAMOJA: MWEZI FEBRUARI .

 


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na watumishi wa ofisi hiyo sambamba na kusheherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa watumishi waliozaliwa mwezi Februari katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma







Keki na Shampeni maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya kusheherekea kumbukizi ya siku za kuzaliwa kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma waliozaliwa mwezi Februari iliyofanyika jana Februari 26, 2025 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma







Baadhi ya wazaliwa wa mwezi Februari wakishirikiana kukata keki kwa niaba ya wenzao wakati wa hafla ya chakula cha pamoja kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambayo kama ilivyo ada huambatana na sherehe hizo kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma.








Baadhi ya wazaliwa wa mwezi Februari wakishirikiana kumlisha keki mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamyule wakati wa hafla ya chakula cha pamoja kwa watumishi wa Ofisi yake kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma.








Picha juu na chini, baadhi ya watumishi wakilishwa keki na mgeni Rasmi wakati wa hafla ya chakula cha mchana cha pamoja kwa watumishi wa ofisi hiyo inayoambatana na sherehe za kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa wazaliwa wa mwezi Februari iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jengo la Mkapa Jijini Dodoma jana Februari 26, 2025.













 Pichani, baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma walioshiriki hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja inayoambatana na shehere za kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa watumishi waliozaliwa mwezi Februari katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa Jijini Dodoma jana Februari 26, 2025.






Na Sofia Remmi.
Habari-RS Dodoma 

Ikiwa ni utamaduni wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kila ifikapo Jumatano ya mwisho wa mwezi,Mkuu wa Mkoa,Menejimenti na Watumishi kukutana na kula chakula cha mchana pamoja na kusheherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa watumishi waliozaliwa mwezi husika,

Jumatano ya Februari 26,2025, Utamaduni huo umeendelezwa ambapo majira ya Saa Saba Mchana, Watumishi wakiongozwa na Mkuu wa Seksheni ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe, Daktari Thomas Rutachunzibwa, wamekutana kwa chakula cha mchana pamoja na kusheherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa watumishi waliozaliwa mwezi Februari,ambapo sherehe hiyo imejumuisha kukata keki pamoja na kufungua shampeni ikiwa ni ishara ya kuwatakia heri wahusika.

Aidha,kama ilivyo ada   chakula hicho cha mchana huambatana na uwasilishwaji wa mada ambazo zimepangwa kwa siku husika,lengo likiwa ni kuwaongezea watumishi maarifa katika nyanja tofauti tofauti.Mwezi huu mada zilikuwa Mbili,ya kwanza ikiwa ni Uongozi na ya pili Itifaki.

#mtiwangubirthdayyangu 
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu



















Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA