VIFAA VYOTE VYA UJENZI VINUNULIWE NA VIWEPO ENEO LA UJENZI-RAS MMUYA.
Na.Sofia Remmi
Habari- RS Dodoma
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar K. Mmuya amefanya ziara ya kukagua miradi ya Kimkakati Katika Halmashauri ya Wilaya za Chemba na Kondoa Mji, Februari 25,2025 .
Katika ziara hiyo Katibu Tawala alitembelea; Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum ya wavulana ya Kanda inayogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4,1000,000,000.Mradi wa Shule Mpya ya Sekondari Kidoka unaogharimu kiasi cha Shilingi 443,597,084 na mradi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Ufundi wa Amali Kata ya Kingale inayogharimu kiasi cha shilingi 544,225,626.00
Akizungumza akiwa katika ziara hiyo, Katibu Tawala Mmuya amesema,
"Mhe.Rais ametoa fedha nyingi kwenye miradi hii ya kimkakati, jukumu lililobaki lipo kwenu la kununua vifaa vyote na viwepo eneo la ujenzi na sio mtu anajiamulia tu kununua vifaa kidogo kidogo,jambo hilo hapana vifaa vinunuliwe vyote.
Mradi hii itakuja kuwasaidia sana Vijana wetu, hivyo muda uliopangwa kukamilisha uzingatiwe, na hatutaki kuona mnavuka kipindi mlichopewa cha kukamilisha.
Fedha zilizoletwa ni nyingi katika miradi hii, hivyo fedha hizo zitumike vizuri ili miradi yote ikamilike kwa weledi na kwa ufanisi,ili vijana wetu waje kunufaika na miradi hii ikiwemo kuwaletea elimu kwa wakati zaidi” amesema RAS Mmuya.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa ndugu Said Majaliwa amesema,
"tutahakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati na kwa weledi ili azma ya Mhe Rais wetu ya kutaka kutatua changamoto kwenye sekta ya Elimu ikamilike kwa weledi zaidi.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
Comments
Post a Comment