WAKULIMA 40,000 WA MTAMA KUNUFAIKA NA MRADI WA CSAP DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, (hayupo pichani) ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Februari 17, 2025 kuhusu Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama.
Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Februari 17, 2025 kuzungumzia utekelezaji wa Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan pamoja na wajumbe wengine walioambatana na Balozi huyowakizungumza kuhusu Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma leo Februari 17, 2025 ofisini kwake jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akimkabidhi zawadi Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, alipotembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Februari 17, 2025 kuzungumzia Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) akiwa na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa WFP Tanzania Ronald Tranbahuy walipotembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Februari 17, 2025 kuzungumzia Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, Mkurugenzi Mkazi wa WFP Tanzania Ronald Tranbahuy na wajumbe wengine walipotembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma leo Februari 17, 2025 kuzungumzia Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ wenye lengo la kuwanufaisha wakulima wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma.
Na. Hellen M. Minja,
Habari – DODOMA RS
Takribani wakulima 40,000 wa zao la Mtama Mkoa wa Dodoma, wanatarajiwa kunufaika na kilimo hicho kutokana na utekelezaji unaoendelea wa Mradi wa ‘Climate Smart Agriculture Project (CSAP)’ ambao ni wa miaka minne (2022-2026) kwa ufadhili wa Irish Aid chini ya Shirika la Chakula Ulimwenguni WFP.
Hayo yamebainishwa na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bi. Nicola Brennan, leo Februari 17, 2025, alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma kumfahamisha maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
Lengo la mradi ni kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,umewekeza zaidi kwenye zao la mtama kutokana na sifa yake ya kuhimili mabadiliko hayo, huku ukilenga zaidi kuwainua wakulima wanawake kiuchumi kwani soko lake linafikia shilingi Bilioni 3.08
Mhe. Senyamule amefurahishwa na utekelezaji wa Mradi huo na ameishuku Serikali ya Ireland kwa ufadhili kwani moja ya vipaumbele vya Mkoa wa Dodoma mwaka huu ni kuinua uchumi wa Wanadodoma, ikizingatiwa kuwa 72% ya wakazi wake ni wakulima hivyo, Mradi huo utasaidia kufikia malengo ya Mkoa kwa haraka.
Vijiji 222 vinavyopatikana katika Wilaya sita (6) za Mkoa wa Dodoma vinatarajiwa kufikiwa na Mradi hadi kufikia 2026 ambapo Mradi utakua umemaliza muda wake. Balozi huyo atatembelea mradi unaotekelezwa kwenye Halmashauri za Chamwino na Bahi.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment