WANUFAIKA WA TASAF DODOMA, WATAKIWA KUTUMIA MIRADI YA MAENDELEO KUJIONGEZEA KIPATO.

 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza na wanufaika wa Mpango wa kusaidia Kaya Masikini Nchini (TASAF) juu ya ajira nyepesi za kujiongezea kipato alipofanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na wanufaika hao katika Kata ya Makutupora, Jijini Dodoma leo Februari 14, 2025.







Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma Mjini Bi. Sakina Mbugi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza na wanufaika wa Mpango wa kusaidia Kaya Masikini Nchini (TASAF) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kutembelea na kuzungumza na wanufaika hao katika Kata ya Makutupora, Jijini Dodoma leo Februari 14, 2025.








Mnufaika wa Mpango wa Kusaidia TASAF Bi. Ester Chitojo, Mkazi wa Mchemwa Jijini Dodoma, ambaye amefanikiwa kujenga nyumba kwa fedha za TASAF akisimulia safari yake ya mafanikio mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule pindi alipomtembelea nyumbani kwake wakati wa ziara yake leo Februari 14, 2025








Nyumba ya Mnufaika wa Mpango wa Kusaidia TASAF Bi. Ester Chitojo, Mkazi wa Mchemwa Jijini Dodoma, ambaye amefanikiwa kuijenga kwa fedha za TASAF kama inavyoonekana wakati alipotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Februari 14, 2025








Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kusaidia Kaya Masikini Nchini (TASAF) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kwa wanufaika hao wa Kata ya Makutupora, Jijini Dodoma leo Februari 14, 2025.




Na. Hellen M. Minja, 

       Habari – DODOMA RS


Wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Nchini (TASAF) Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kutumia fursa za ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo iliyoletwa na Daktari Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kujiongezea kipato ili kufikia malengo ya Mkoa ya kuinua uchumi na kuondoa umasikini.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo leo Februari 14, 2025 alipofanya ziara ya kutembelea na kuzungumza na wanufaika wa Mpango huo katika Kata ya Makutupora Jijini Dodoma.

“Mhe. Rais amefanya vitu vingi hasa kwetu Dodoma, upande wa elimu, afya na miundombinu mikubwa. Hivi vitu vinamhusu kila mmoja, unaweza usipande hiyo ndege lakini uwanja ule na ndege kuwepo pale, ukakusaidia wewe kupata hela.Unaweza usipite na gari kwenye barabara ya Mzunguko,lakini uwepo wa barabara hiyo ya Mzunguko ukakusaidia kupata hela.Mwaka 2025 ni mwaka wa kuondoa umasikini kwa kutumia fursa za miradi hii” Mhe. Senyamule 

Mbali na kuzungumza hayo, Mhe Senyamule aliwapa nafasi wanufaika hao kutoa kero zinazowakabili ambapo mmoja kati yao aliwasilisha kero inayohusu kupitisha fedha za ruzuku kwa njia ya benki ambapo inawalazimu kutumia nauli kufuata fedha hizo.

Akijibu kero hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema kwa sasa juhudi zinafanyika ili fedha hizo ziwe zinatolewa kupitia Mawakala wa benki ambao wapo karibu na wanufaika kwani njia hiyo ni salama kuliko kupewa fedha mkononi hivyo, amewataka wanufaika hao kuwa wavumilivu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule amemtembelea mnufaika wa TASAF Bi. Ester Chitojo katika eneo la Mchemwa Jijini humu aliyefanikiwa kujenga nyumba ya makazi kwa fedha alizozipata kwa kuzizalisha zaidi.

“Kupitia fedha nilizokua nikipokea, nilifanikiwa kununua mbuzi wawili, mbuzi hao walizaa,baadae nikabadilisha kwa ng’ombe wawili, ng'ombe wakazaa wakafika 12, nikauza 4, nikapata fedha za kuanza ujenzi wa nyumba hii ya vyumba vitatu vya kulala, pia nafanya kilimo cha choya ambacho kinanisaidia kupata fedha za kujikumu na familia yangu”.

Mradi mwingine wa TASAF uliotembelewa na Mkuu wa Mkoa huyo ni Mradi wa kutengeneza matofali madogo (pavements) ambao unalengo la kutengeneza ajira ya muda kwa wanufaika wa Kata ya Kiwanja cha Ndege na umenufaisha Kaya 45 zilizokua na vigezo.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni miongoni mwa Halmashauri zinazonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) awamu ya tatu sehemu ya pili, unaotekelezwa katika Kaya 41 za Jiji hili katika mitaa 192 ikiwa na jumla ya Kaya 5,773 zenye jumla ya wanufaika 19,437 ambapo wanawake ni 11,531 na wanaume 7,906.



#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu









Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA