EACOP WAASWA KUACHA ALAMA KWA WANANCHI WANAOPITIWA NA MRADI

 




















 

 Na. Hellen M. Minja,

Habari – DODOMA RS

Uongozi unaosimamia Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kipande cha Dodoma, umesisitizwa kuzingatia sheria ya kurudisha kwa jamii kupitia Mradi huo unaotekelezwa katika kijiji cha Seria, Kondoa na Wilaya ya Chemba kwani wananchi wanatakiwa kuona alama iliyoachwa na mradi unaopita kwenye maeneo yao.

Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na uongozi huo pindi ulipotembelea ofisini kwake Jengo la Mkapa Jijini Dodoma Machi 28, 2025 kwa lengo la kuwasilisha maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo.

“Mnaweza kuweka kisima na zile njia za umwagiliaji, utakuta hata sehemu ya heka 100 inamwagiliwa sehemu moja, matokeo yake yatakua makubwa na kisima kitadumu muda mrefu na ndio mwelekeo wa Serikali na Wizara ya Kilimo tupate kilimo cha muda mrefu na si kutegemea mvua. Kwa sababu hiyo, pamoja na yote, nendeni mkafanye hivyo”.

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amesema Mkoa wa Dodoma umejikita katika kukuza hali ya uchumi kwenye ngazi ya familia hivyo jitihada za mradi na Mkoa zinatakiwa ziwe kitu kimoja kuimarisha kilimo na upandaji miti ya matunda hasa kwenye eneo la mradi.

Hatahivyo, taarifa ya Mradi inaonesha utekelezaji wake unaendelea vizuri katika utekelezaji wa Mikakati waliyojiwekea ambayo ni uboreshaji kilimo, ufugaji na kuwajengea uwezo wananchi katika masuala ya ujasiriamali. Kwa upande wa stahiki kwa waguswa, Mkoa wa Dodoma una waguswa 842 lakini wanaostahili uwezeshaji ni 700 kwa kutoa Taasisi kwani Mpango huo unakwenda kwenye Kaya.

Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) litakua na urefu wa Km 1,443 litakapokamilika kutokea Kabaale-Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, nchini Tanzania ambapo litakua na uwezo wa kusafirisha mafuta ghafi lita za ujazo 34,339,248 (216,000 bopd) kwa siku na utekelezaji wake kwa Mkoa wa Dodoma umefikia 56% ukihusisha ujenzi wa Makambi. 


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA