LISHE BORA : KICHOCHEO CHA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA JAMII

 















Na Sofia Remmi.
Habari Dodoma RS 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, ameiasa jamii kuzingatia suala la lishe Bora kutokana na umuhimu wake. 

Mhe Senyamule ametoa kauli hiyo wakati akiendesha kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa  Lishe  kwa Kipindi cha Julai- Disemba 2024.

Kikao hicho kimefanyika  Machi 28,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma (Manispaa ya Zamani).

"Lishe ni jambo muhimu, tukifanikiwa watu wakaelewa vizuri kuhusu lishe,wale vizuri,watu wakila vizuri,mengine yote yatakaa vizuri" Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Awali akifungua kikao hicho, Mhe.Senyamule amesema 
ni dhahiri kuwa, lishe bora katika jamii ni kichocheo cha maendeleo endelevu katika nyanja zote na hasa ya viwanda, afya, kilimo, elimu, biashara, uchumi.

“Athari za lishe duni au utapiamlo zitakapodhibitiwa au kutokomezwa ndipo malengo ya maendeleo katika nyanja hizi yataweza kufikiwa kwa ufanisi. Tafiti ya kidemografia ya mwaka 2022”

“Wataalam wetu kupitia tafiti mbalimbali walibaini afua kadhaa ambazo iwapo zitafanyiwa kazi zinaweza kubadili hali iliyopo kwa sasa. Afua hizo, ziliandaliwa mkakati wa utekelezaji kwa mfumo wa mkataba. Kama nilivyoeleza hapo awali.” Amesema Senyamule 

Kwa upande wake Afisa Lishe Mkoa Bw.Ally Mvungi amesema Mkoa unafikia malengo yaliyotarajiwa katika Halmashauri zote kwa kufanya vizuri kwenye  utekelezaji wa afua za lishe.

“Jamii kuhusishwa katika kupewa Elimu kuhusu matumizi ya vyakula vya asili vyenye virutubisho kwa Wingi ili kuhamasisha afya na lishe bora”amesema Mvungi.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA