RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA WENYE UHITAJI DODOMA

 


Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule akiwashukuru na kuwapongeza walezi wanaolea watoto kwenye vituo vya mahitaji maalum wakati alipokwenda kutoa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodoma Machi 30, 2025






Kiongozi wa Kijiji cha Matumaini Padri Vicent Boselli akizungumzia namna kituo chake kinavyolea watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 20 sasa wakati Mhe. Senyamule alipokwenda kutoa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodoma Machi 30, 2025











Picha juu na  chini ni baadhi ya watotyo wanaolelewa kwenye kituo cha KIjiji cha Matumaini walipotembelewa na Mh. Senyamule kwa ajili ya kupewa zawadi za mkono wa Eid zilizotolewa na  Mhe. Rais Samia kwenye vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center Jijini Dodoma Machi 30, 2025









Na;Happiness Elias Chindiye 

Habari - Dodoma RS


Mkuu Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Machi 30,2025 amekabidhi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suhulu Hassan, zawadi za mkono wa Eid kwenye vituo vya kulea watoto wenye mahitaji maalum. 

Mhe.Senyamule amekabidhi zawadi hizo zilizotolewa na Mhe. Rais kwa walezi na viongozi wa vituo vya Kijiji cha Matumaini na Rahman ‘Orphanage Center ‘vilivyopo Jijini Dodoma.

“Kwa niaba ya Serikali, niendelee kuwashukuru na kuwapongeza walezi wote mnaolea watoto kwenye vituo hivi, Mungu awabariki kwa upendo mnaouonesha kwa watoto hawa” Mhe. Senyamule

Naye Kiongozi wa Kijiji cha Matumaini Padri Vicent Boselli amesema kwa zaidi ya miaka 20 kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto wenye maambukizi ya VVU na kuwapa matumaini ya upendo na kuishukuru Serikali kwa kuwakumbuka kwenye kipindi hiki cha Sikukuu.

Kwa Upande wao Shadrack Hassan na Hazla Ramadhan ambao ni miongoni mwa watoto wenye mahitaji wanaolelewa katika vituo hivyo wamemshukuru Mhe. Rais pamoja na Uongozi wa Mkoa kwa zawadi hizo.

Zawadi zilizotolewa ni pamoja na mchele, Mbuzi , juisi, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage na mahitaji mengine muhimu.


#keroyakowajibuwangu

#dodomafahariyawatanzania

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA