RC SENYAMULE AWASHUKURU WANADODOMA KWA UPENDO NA USHIRIKIANO KWAKE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwashukuru Wanadodoma kwa upendo na Ushirikiano wanaomuonesha wakati wa hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa makundi maalum ya kijamii Mkoani hapa Machi 27, 2025
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya akijumuika na viongozi wengine wa Mkoa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa.
Kaimu Kadhi wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Nurdin Ramadhan, akimshukuru Mhe. Senyamule na kuwaasa Wanadodoma kumuombea dua kwa Iftar aliyoiandaa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa.
Baadhi ya makundi maalum yanayopatikana katika Mkoa wa Dodoma yakijumuika kwenye Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa kwa makundi maalum ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa kwenye picha za pamoja na makundi mbalimbali yaliyoshiriki Iftar aliyoiandaa kwa makundi hayo ya kijamii Machi 27, 2025 katika viwanja vya makazi yake Kilimani, Jijini hapa.
Na. Hellen M. Minja,
Habari - DODOMA RS
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesifu na kushukuru upendo wa Wanadodoma kwake tangu kukasimiwa madaraka ya kuuongoza Mkoa huu mpaka sasa. Ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha makundi mbalimbali katika Jamii ya Dodoma Machi 27, 2025 kwenye viwanja vya Makazi yake Kilimani, Jijini Dodoma.
Mhe. Senyamule amesema; "Nitoe shukrani kwenu, muda wote ambao tumekaa pamoja, mmenipa Ushirikiano mkubwa sana, tumefanya kazi na kuishi kwa upendo sana bila kujali tofauti zetu za Imani, makabila wala vyama. Hii ni kwa sababu nyote mpo tayari kushirikiana kulinda Umoja wa Kitaifa na wanadodoma na wote tunataka maendeleo ya Dodoma." Mhe. Senyamule.
Kadhalika akizungumza katika shughuli hiyo, Kaimu Kadhi wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Nurdin Ramadhan, amemshukuru Mhe. Senyamule kwa jambo hilo jema mbele za Mungu ambalo linapaswa kufanywa na kila mwenye uwezo na kuwasihi wananchi wa Mkoa huu kumuombea Dua njema kwa sadaka hiyo hasa katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.
Utaratibu huo umekua endelevu wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, kuandaa Iftar kwa Makundi mbalimbali ya kijamii katika Mkoa wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo Makundi hayo hupata fursa ya kujumuika pamoja na kupata mawaidha yenye kujenga Kiimani.
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirrhdayyangu
Comments
Post a Comment