VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA

 























Na; Happiness E. Chindiye
      Habari - Dodoma Rs 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara Ndugu, Stephen Wasira ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa Nchini kuheshimu Misingi ya Utawala bora na Demokrasia ikiwa ni pamoja na kutoingilia mienendo ya Mashauri yaliyo kwenye vyombo vya dola ili kuruhusu haki kutendeka kwa uhuru.

Wasira ametoa wito huo jijini Dodoma Leo Aprili 25,2025 wakati akizungumza na wanachama na wananchi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/25.
 
“Viongozi wa siasa heshimuni utawala na demokrasia ili kusaidia vyombo vya dola kufanya maamzi kwa uhuru”. Wasira

Naye ,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule ameeleza kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi ikiwamo kero ya Maji katika jiji la Dodoma.

Katika ziara hii Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Stephen Wasira Jijini Dodoma ametembelea miradi ya miundombinu ya Afya, Kituo cha Afya Ilazo na kiwanja cha ndege cha Kimataifa Msalato pamoja na kupanda mti Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya kukijanisha Dodoma.



#keroyakowajibuwangu
#dodomafahariyawatanzania




















Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA