YALIYOJIRI; MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA WILAYA YA BAHI
Katika siku ya kihistoria ya tarehe 25 Aprili 2025, Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi umbali wa Kilometa 164 ambapo ulipitia miradi 6, yenye thamani ya shillingi 1,517,657,312.63 .Miradi hiyo ni kama ifuatavyo;
Ujenzi wa Daraja la Mgondo, Barabara ya Zamahero - Asanje - Kogogo,ulizinduliwa rasmi na unagharimu shilingi 153,559,166.3. Daraja hili litasaidia kuboresha usafiri na ushirikiano kati ya vijiji vinavyopitiwa na barabara hii.
Ujenzi wa Miundombinu ya Afya na Usafi wa Mazingira katika Zahanati ya Mayamaya,Mwenge ulitembelea mradi huu wenye thamani ya shilingi 52,000,000. Ujenzi huu ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa eneo hilo.
Kikundi cha Vijana Maua Zanka .Mradi huu wenye thamani ya shilingi 20,000,000 ulitembelewa na Mwenge. Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwajengea uwezo vijana katika shughuli za kiuchumi.
Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kisima cha Ndege.Mwenge uwekea jiwe la msingi katika mradi huu wenye thamani ya shilingi 547,225,626. Shule hii itasaidia katika kuongeza fursa za elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo.
Mradi wa Nishati ya Gesi Shule ya Sekondari Mundemu.Mradi huu wenye thamani ya shilingi 35,555,100 unalenga kuboresha upatikanaji wa nishati safi katika shule hiyo, hivyo kusaidia utunzaji wa mazingira na kuondoa mazingira magumu ya utendaji kazi kwa wapishi.
Mradi wa Usambazaji wa Maji katika Kijiji cha Ibihwa.
Mwenge ulizindua mradi huu wa maji wenye thamani ya shilingi 709,317,420.,utawezesha upatikanaji wa maji safi na salama,ambayo ni muhimu kwa afya na ustawi wa jamii.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa nishati safi ya gesi katika shule ya Sekondari Mundemu,Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Ismail Ally Ussi alisema;
"Mhe. Rais Daktari Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Wilaya zote,kata zote,vijiji vyote na mikoa yote, ihamasishe juu ya utumiaji wa nishati safi na salama.Wanafunzi wetu wa Mundemu kwa kushirikiana na Walimu na uongozi wa Halmashauri pamoja Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wameutendea haki na wameupa heshima Mwenge wetu wa Uhuru kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma
Comments
Post a Comment