YALIYOJIRI;MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA
Na Francisca Mselemu
Habari - Kondoa DC
Tarehe 23 Aprili 2025,Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa umbali wa kilometa 154.9.
Katika mbio hizo, mwenge ulipitia miradi 7 yenye manufaa kwa jamii, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha maendeleo na kuonyesha juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha maisha ya wananchi.Miradi hiyo ni ;
Mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Zahanati ya Itundwi.Ulizinduliwa, Gharama shilingi 50,000,000, mradi huu unalenga kuboresha upatikanaji wa maji safi ili kuimarisha usafi wa mazingira ya eneo hilo .
Mradi wa matumizi ya Nishati Safi. Ulikaguliwa, gharama, shilingi 5,000,000,unahusisha matumizi ya nishati mbadala, kusaidia kupunguza utegemezi wa nishati zisizokuwa rafiki kwa mazingira na afya za watumiaji.
Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Filimo.Uliwekewa jiwe la msingi, gharama, shilingi 32,549,053.9 utasaidia katika usimamizi wa shughuli za kijiji na kuimarisha utawala bora.
Ujenzi wa Vyumba Vinne vya Madarasa na Matundu 8 ya Vyoo.Ulizinduliwa, gharama,shilingi 103,200,000.Mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoweza kupata elimu bora.
Ujenzi wa Daraja la Mto Hurui.Ulizinduliwa, gharama shilingi 1,626,281,990.
Daraja hili litawawezesha wananchi kuvuka mto bila kupata changamoto yoyote,na kuunganisha maeneo mbalimbali, hivyo kurahisisha usafiri na biashara.
Mradi wa Kikundi cha Vijana Disa (Vijana Electronics)ulikaguliwa, gharama shilingi 10,000, mradi huu unalenga kuwasaidia vijana kujiajiri.
Mradi wa usambazaji wa Maji Bambare.Ulizinduliwa, gharama shilingi 1,270,494,630. Mradi huu unakusudiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa eneo hili, kuboresha afya na maisha yao.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zilikuwa ni fursa nzuri ya kuonyesha juhudi za serikali na wadau wengine katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali.
Akizungumza Kwa nyakati tofauti na Wananchi waliokusanyika katika maeneo ya miradi,kuupokea na kuushangilia Mwenge wa Uhuru,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Ismail Ali Ussi amesema;
" Mimi na vijana wenzangu watano tumejionea mambo makubwa yaliyofanywa na Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hassan,fedha nyingi zimetumika,ninachowaomba Wananchi,tumuunge mkono Rais wetu kwa kushiriki kutunza miradi hii ili iweze kutimiza dhamira yake njema,na mapenzi mema aliyonayo kwa wananchi wake".
Comments
Post a Comment