YALIYOJIRI;MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA

 

















Na Francisca Mselemu
       Habari – Mpwapwa DC

Tarehe 27 Aprili 2025, Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe na ari kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kukimbizwa umbali wa kilometa 234 .

 Katika mbio hizo, miradi  8 yenye thamani ya jumla ya shilingi 1,118,248,505.34,ikionesha maendeleo makubwa yanayofanyika katika sekta mbalimbali za maendeleo ya jamii.

Moja ya miradi muhimu ni ujenzi wa karakana ya vifaa vya kilimo katika Kijiji cha Ngh’ambi,ulizinduliwa,  gharama za mradi huu ni shilingi 55,790,000. Hii ni juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza tija kwa wakulima wa eneo hilo.

Pia, zahanati ya  Kijiji cha Ngh’ambi iliwekewa jiwe la msingi kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya afya,  gharama za mradi huu ni shilingi 65,000,000, ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha huduma za afya kwa Wananchi wa Kijiji hicho.

Katika sekta ya miundombinu, ujenzi wa daraja jipya la Chifu Mkunda mjini Mpwapwa umefanyika, gharama za mradi huu ni  shilingi 130,340,000, ili kurahisisha usafiri na kuimarisha usalama wa wananchi wanaosafiri kupitia eneo hilo.

Mwenge wa Uhuru  pia ulitembelea shughuli za kikundi cha uuzaji wa mabegi na mikoba Mjini Mpwapwa, mradi unaoonyesha nguvu na ujasiri wa wananchi kutengeneza kipato,gharama za mradi huu ni  shilingi 8,850,000.

Miradi mingine ni ujenzi wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mgoma-Godegode,uliotekelezwa kwa shilingi 109,200,000, na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari George Simbachawene.Gharama za mradi huu ni shilingi 547,825,626, ikiwa ni juhudi za Serikali kuimarisha elimu kwa watoto wa eneo hilo.

Aidha, zahanati ya Mkoleko  imefunguliwa rasmi, ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma za afya na gharama yake ni shilingi 57,500,000. 

 Ofisi ya Afisa Tarafa Rudi ilizinduliwa,ujenzi wa ofisi hii umegharimu shilingi 143,742,879.34, ukionyesha juhudi za Serikali katika kuimarisha huduma za kijamii na utawala bora.

“Lakini niwashukuru ndugu Wananchi wa neo hili kwa kuonesha  Upendo kwa Rais wetu, kwa sababu  leo hii Mwenge wa Uhuru umekuja kujionea  shule bora  na ya kisasa ambayo kwa kweli  inakwenda kutatua changamoto juu ya watoto wetu katika maeneo haya.Hii ni faraja kubwa na upendo  ambao mmeuonyesha, mngeweza  kumwambia Mbunge wenu kwama sisi hatutaki shule hapa,shule isingejengwa .Huku ni kuunga mkono juhudi za Daktari Samia Suluhu Hassan”.Alisema Kiongozi wa mbio za Mwenge,ndugu Ussi.
















Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA