KAMPENI YA ‘GURUDUMU LA MAMA SAMIA’ - MATOKEO YA IMANI YA SERIKALI KWA SEKTA BINAFSI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza na Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mkurugenzi wa Kampuni ya 'Road Master Bw. Fuein Makamba akizungumza na Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni yake na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Pikipiki Jijini Dodoma (UMAPIDO) Bw. Chacha Marwa akizungumza na Maafisa Usafirishaji wenzake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi magurudumu mapya ya Pikipiki kwa baadhi ya Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda kama ishara ya uzinduzi wa Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akifurahi pamoja na Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua rasmi Kampeni ya 'Gurudumu la Mama Samia' iliyoanzishwa na Kampuni ya 'Road Master' na kufanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma Mei 28, 2025.
Na. Hellen M. Minja
Habari – DODOMA RS
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kutengeneza mazingira rafiki kwa Sekta Binafsi kujenga imani kubwa kwa Serikali hasa linapokuja suala la mikopo ambapo kampuni ya ‘Road Master’ kupitia kampeni ya ‘Gurudumu la Mama Samia’ inakopesha magurudumu ya Pikipiki kwa gharama nafuu na kwa malipo kidogo kidogo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo leo Mei 28, 2025 alipokua akizindua Kampeni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya soko la Machinga lililopo ‘Bahi Road’ Jijini humu ambapo magurudumu hayo yanakopeshwa kwa Maafisa usafirishaji wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda.
“Sekta binafsi zimejenga Imani kubwa kwa Serikali kwa sababu ya dhamira ya Mhe. Rais kuwa yapo mambo ambayo yanatakiwa yafanywe na sekta binafsi lakini, ili sekta binafsi awe na Imani kuwa bodaboda nitawakopesha na kuwa amini kabla hajamaliza kulipa hela ni lazima itengeneze mazingira mazuri”.
Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa kuendelea kujitoa kila wakati kusaidia wananchi wake kwani usaidizi huo, unakwenda kuokoa maisha na kuimarisha biashara za vijana hao siku za usoni.
Hata hivyo, Mbunge huyo amesema, kampeni hiyo imeridhiwa na Mhe. Rais kwa kuwagusa waendesha Bodaboda na Bajaji nchi nzima kwa kutambua changamoto kubwa waliyonayo ya upatikanaji wa matairi mapya kwa wakati, ikilenga kuwapunguzia mzigo vijana hao na mpango huo utaamsha ari ya vijana wengi kuzingatia sheria na kufuata taratibu hivyo kupunguza ajali za barabarani.
Naye, Mkurugenzi wa ‘Road Master’, Kampuni iliyoanzisha kampeni hiyo Bw. Fuein Makamba amesema kampuni yake imeitikia wito wa kumuunga mkono Mhe. Rais kupitia uwezeshaji wa haki za vijana hasa kundi la bodaboda na bajaji nchini kwani kupitia uwezeshaji huo, imeanzisha kampeni hiyo yenye lengo la kuchochea maendeleo ya vijana hao Mkoani hapa.
Kupitia Mpango huo, Afisa usafirishaji wa Bodaboda au Bajaji ambaye atahitajika kununua tairi mpya lakini hana fedha kwa wakati mmoja, kupitia mpango huo ataweza kutoa shilingi 10,000 akapata tairi mpya ya shilingi 70,000 na fedha iliyobaki atailipa kidogo kidogo kwa siku 30 awe amemaliza kiasi chote kinachohitajika.
#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment