TIMU YA UMITASHUMTA 2025 MKOA WA DODOMA YASISITIZWA NIDHAMU,UPENDO NA KUJITUMA
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Justin Machela, akihamasisha timu ya UMITASHUMTA Mkoa kuwa na nidhamu, upendo na kujituma wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu ya Mkoa itakayowakilisha kwenye mashindano hayo Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Afisa Michezo Mkoa wa Dodoma Bw. Evance Sangawe akitangaza majina ya wanamichezo watakao wakilisha Mkoa kwenye michezo ya UMITASHUMTA 2025 Kitaifa Mkoani Iringa wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wakuu Tanzania (TAPSHA) Mwalimu James E. Manary akizungumzia msaada walioutoa kuunga mkono juhudi za Mkoa katika kuhudumia kambi ya timu ya UMITASHUMTA 2025 wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu hiyo itakayowakilisha Mkoa kwenye mashindano hayo Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki kwenye mchakato wa kupata timu ya Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu hiyo itakayowakilisha kwenye mashindano UMITASHUMTA 2025 Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Makombe yaliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kwenye mchujo wa kupata timu ya Mkoa wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu hiyo itakayowakilisha kwenye mashindano ya UMITASHUMTA 2025 Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Baadhi ya washindi wa michezo tofauti tofauti wakikabidhiwa makombe na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Justin Machela,wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu ya Mkoa itakayowakilisha kwenye mashindano ya UMITASHUMTA 2025 Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Afisa elimu awali na msingi Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mwl. Josephat Ambilikile (katikati), akiwa ameshikilia Kombe la Mshindi wa jumla ambalo limeenda kwa Halmashauri hiyo wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu ya Mkoa itakayowakilisha kwenye mashindano ya UMITASHUMTA 2025 Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma leo Mei 30, 2025.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Justin Machela (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa TAPSHA Mwalimu James E. Manary ambao wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Mkoa kuwahudumia wanamichezo wa timu ya Mkoa ya UMITASHUMTA 2025 iliyoweka kambi kwenye shule ya sekondari Dodoma Mei 30, 2025
Na. Hellen M. Minja
Habari – DODOMA RS
Wawakilishi wa timu ya Mkoa wa Dodoma kwenye Umoja wa Michezo kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2025 inayotarajiwa kufanyika Mkoani Iringa, wametakiwa kuliheshimisha jina la Mkoa kwa kuwa na nidhamu, kupendana na kujituma ili kuhakikisha makombe yote yanarudi Dodoma.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Dodoma ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Justin Machela, ameyasema hayo Mei 30, 2025 wakati wa hafla fupi ya kutangaza timu ya Mkoa itakayowakilisha kwenye mashindano hayo Kitaifa Mkoani Iringa iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Dodoma.
“Makombe yanapatikana kwa namna tatu, kujituma sana uwanjani, nidhamu na kupendana ninyi kwa ninyi. Mkuu wa Mkoa anatamani kila tunaposhindana Dodoma tuwe wa kwanza kwa vigezo na viwango vya hali ya juu. Waalimu ambao tunakwenda na watoto, kazi yetu ni kuwasimamia na kuendelea kuwafundisha, kuhakikisha nidhamu ya watoto inakua juu na ya yetu pia inakua juu”.
Kadhalika, Umoja wa Walimu Wakuu Tanzania (TAPSHA) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mwalimu James E. Manary, wameunga mkono juhudi za kuwawezesha watoto hao kukaa kambini kwa kipindi ambacho wanasubiri safari ya kuelekea Iringa kwa kutoa vyakula na fedha taslimu.
“Sisi vijana wa TAPSHA, tunakabidhi vitu vyenye thamnai ya shilingi 3,380,000 ambavyo ni vyakula, jezi za ‘football’ 22, jezi za ‘netball’ 10 lakini pia ‘tracksuit’ ambazo tumezitoa kama motisha kwa mtoto atakayefanya vizuri pia tunatoa fedha taslimu shilingi 730,000 ambazo 600,000 kwa ajili ya nyama na 130,000 ya vitafunwa”.
Katika hatua nyingine, Afisa elimu awali na msingi Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mwl. Josephat Ambilikile, amezungumzia siri ya mafanikio ya Chemba kwani wamebeba vikombe vingi sambamba na kuibuka washindi wa jumla kwenye mashindano hayo ngazi ya Mkoa ambapo amesema ni ushirikiano mkubwa ulipo katika idara ya elimu Msingi na jitihada za Walimu shuleni.
Mashindano ya kutafuta timu ya Mkoa kwa ajili ya kushiriki UMITASHUMTA 2025, yameshirikisha wanafunzi 960 kutoka shule za msingi za Halmashauri zote 8 za Mkoa wa Dodoma ambapo mchujo ulifanyika na kupatikana wanafunzi 120 kwenye timu hiyo ya michezo mbalimbali ambao watakaa kambini hapo kwa siku 6 kabla ya kuelekea Mkoani Iringa.
#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment