VITUO VYA ‘KILIMO ANGA’ NCHINI, KUPATA NDEGE MPYA ZA KUDHIBITI VISUMBUFU VYA MIMEA

 


Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe,akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara yake kuhusu kufanyika mchakato wa ununuzi wa Ndege tatu za kudhibiti visumbufu vya mimea wakati wa hafla ya kupokea ndege moja iliyonunuliwa kwa lengo hilo leo Mei 30, 2025 kwenye Kiwanja kidogo cha Ndege Jijini Dodoma.







Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiishukuru Wizara kwa ununuzi wa ndege ya kudhibiti visumbufu vya mimea wakati wa hafla ya kupokea ndege moja iliyonunuliwa kwa lengo hilo leo Mei 30, 2025 kwenye Kiwanja kidogo cha Ndege Jijini Dodoma.







Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe akikagua ndege mpya iliyonunuliwa na Serikali kwa lengo la kudhibiti visumbufu vya mimea wakati wa hafla ya kupokea ndege hiyo iliyofanyika leo Mei 30, 2025 kwenye Kiwanja kidogo cha Ndege Jijini Dodoma.








Viongozi wa dini na baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya kupokea ndege moja iliyonunuliwa kwa lengo la kudhibiti visumbufu mimea leo Mei 30, 2025 kwenye Kiwanja kidogo cha Ndege Jijini Dodoma.






Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (walioketi katikati) katika picha ya pamoja mbele ya ndege hiyo na viongozi waliohudhuria hafla ya kupokea ndege moja iliyonunuliwa kwa lengo la kuthibiti visumbufu mimea leo Mei 30, 2025 kwenye Kiwanja kidogo cha Ndege Jijini Dodoma.




Na. Hellen M. Minja
       Habari – DODOMA RS

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Wizara yake kuanza mchakato wa ununuzi wa ndege mpya tatu kwa ajili ya  vituo vya Kilimo Anga vya kanda vilivyopo katika mikoa ya Arusha,Mbeya na Mwanza lengo likiwa ni kudhibiti visumbufu vya mimea.

Maelekezo hayo ameyatoa wakati wa hafla ya mapokezi ya ndege moja ya kudhibiti visumbufu vya mimea iliyonunuliwa na Serikali chini ya Wizara hiyo kwenye Kiwanja kidogo cha ndege Mkoani Dodoma Mei 30, 2025 ambayo itatumika katika kituo cha Kanda ya Kati.

“Vituo vyote hivi vinatakiwa viwe vina ndege na ‘drones’ kwa hiyo, mchakato wa kununua ndege tatu nyingine uanze sasa hivi. Ni lazima kama Nchi ijitegemee, dunia ya kubebana haipo. Lazima tuweze kutoa huduma, tumeshaanza kununua ‘drones’ za kufanya ‘survilence’, mwaka huu tunanunua drone kwa ajili ya ‘spraying’.” Mhe. Bashe.

Kadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru, amesema ndege hiyo inalenga kuleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo kwa kuleta tija, ajira na kupanua masoko lakini pia kuimarisha hali ya chakula hapa nchini na kuongeza kuwa visumbufu vya mimea ni moja ya jitihada za Mamlaka katika kuleta tija kwenye sekta hiyo. 

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa ununuzi wa Ndege hiyo ambayo italeta matumaini kwa Mkulima.

“Utashi huu unakwenda kuleta matumaini kwa Mkulima ambaye si mvivu, kwani amelima na kutunza mazao yake halafu mwishoni ndege anakula. Kwa Mkoa wa Dodoma itatuongezea upatikanaji wa chakula na wale wavivu sasa wataanza kulima kwani Dodoma pia tunapata athari ya Nzige maeneo ya Bahi na Kwelea kwelea maeneo ya Chemba, Kondoa na Kongwa.”

Ndege hiyo aina ya ‘Thrush 510 P2’iliyonunuliwa kwa gharama ya Shilingi 6,000,000,000 ina uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya saa 4 kutokana na tenki lake kubeba mafuta yenye ujazo wa lita 863, uwezo wa kubeba viuatilifu lita 1,930 uwezo wa kufanya udhibiti kwenye eneo la ekari 2400 kwa mara moja huku ikiwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kutolea takwimu zinazowezesha mpango wa uthibiti wadudu na ndege waharibifu wa mazao na mimea.

#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu












Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA