WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA
Na. Hellen M. Minja
Habari – DODOMA RS
Ikiwa ni siku moja tu baada ya ziara ya Kidiplomasia (Capital City Diplomatic Tour) iliyowahusisha mabalozi kutoka nchi mbalimbali Duniani Jijini Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea ugeni kutoka nchini Dubai kuzungumzia juu ya upatikanaji wa fursa za uwekezaji wa ardhi kwa ajili ya kujenga viwanda kwa kuzingatia Dodoma inazidi kukua kutokana na hadhi yake ya Makao Makuu ya nchi na kupokea wageni wengi wa ndani na nje ya nchi.
Wawekezaji hao ambao ni Bw. Emmanuel Salinos na Bw. Walid Jumaa, wamefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma Mei 28, 2025 ambapo hii ni mara ya pili kufika hapa kwa ajili ya dhumuni hilo ingawa awali waliona Dodoma haijakua kama ilivyo sasa.
Aidha, lengo hasa la wawekezaji hao ni kutafuta eneo lenye ukubwa wa ekari 1,000 kwa ajili ya kuwekeza na kutengeneza Mji unaofanana na Dubai ambapo wataleta wawekezaji wengine kutoka nchini mwao kwani wanaotaka kutengeneza eneo la uwekezaji wa Viwanda.
Mhe. Senyamule amewakaribisha Dodoma na kuwaambia kuwa ipo kwa ajili yao na pindi watakapokua tayari wakaribie huku akiwaeleza kuhusu ziara ya Mabalozi iliyofanyika Jijini hapa Mei 27, 2025 yenye lengo la kuwavutia kuwekeza.
“Jana tulikua na Mabalozi tukiwaonesha fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa, na wameona maendeleo ya Dodoma ambayo hawakuyaona kabla. Kuna mpango wa Balozi zote kuhamia Dodoma kutoka Dar Es Salaam sasa,
Kila tunapowauliza lini mtakuja Dodoma wanasema bado hakuna huduma bora za afya, elimu lakini jana tuliwatembeza kwenye huduma hizo na tuna kauli mbiu ya ‘Dodoma tupo tayari kwa ajili yenu’ wameahidi kuzishawishi Balozi zao kujenga ofisi hapa”. RC Senyamule.
#takedodomatotheworldandbringtheworldtododoma
#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu
Comments
Post a Comment