RC SENYAMULE AZINDUA JENGO LA KUPUMZIKIA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA
Na: Sofia Remmi
Habari:DodomaRs
Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua Jengo la kupumzikia ndugu wa wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Leo tarehe 25 Juni 2025 Katika Viwanja vya Hospital hiyo Jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa Hotuba yake Mhe. Senyamule amewataka wadau wengine wa Serikali na ambao sio wa Serikali kuendelea kuunga Mkono Jitihada mbalimbali za Kiserikali kama alivyofanya Waziri wa Madini na Mbunge wa Jiji la Dodoma Mhe. Mbunge Anthony Mavunde kwa kufanya Ukarabati katika jengo la kupumzikia ndugu wa Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.
"Nitoe wito kwa Wadau wengine waendelee kujitokeza kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kama alivyofanya Mbunge".
Kadhalika, Mhe. Senyamule, amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kuendelea kuchapa kazi zaidi ili huduma ziendelee kuwa bora.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma amemshukuru Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kwa kufanya Ukarabati mkubwa wa Jengo la Kupumzikia Ndugu wanaosubiri Wagonjwa.
"Tunaamini huduma ni nzuri na hili jengo ni msaada mkubwa sana kwa wateja wanaosubili ndugu zao wakati huduma zinaendelea".amesema Dkt.Ibenzi.
Comments
Post a Comment