SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

 




















     Na. Happiness E. Chindiye

     Habari - Dodoma RS 

Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi madhubuti wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kuleta maendeleo edelevu katika taifa la Tsnzania, ikiwemo kuboresha na kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara Nchini. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule wakati akifunga maadhimisho ya kitaifa ya udhibiti wa bidhaa bandia Duniani yaliyofanyika katika ukumbi  wa Mabele Jijini Dodoma. Tarehe 25.06.2025.

“Kupitia uwezeshaji wa Serikali kwa wananchi waliojiunga kwenye vikundi na kupatiwa mikopo katika ngazi mbalimbali, zikiwemo Mikoa na Wilaya, vikundi vya uzalishaji vinaendelea kupata nguvu ya kutengeneza bidhaa zilizo halisi na bora, baada ya kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kutoka SIDO, TBS, BRELA na FCC.

“Serikali kuendelea kuiamini na kuiwezesha Tume ya Ushindani kusimamia usalama wa soko, utimamu wa miliki-bunifu za bidhaa na kumlinda mlaji dhidi ya athari za bidhaa bandia.” - ameeleza Mhe. Senyamule 

Hata hivyo amezielekeza Halmashauri za Mkoa huu kushirikiana na FCC katika kutoa elimu kwa vikundi kuhusu athari za bidhaa  bandia .

“Ili kuleta uendelevu wa mafanikio haya, nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Dodoma kushirikiana na FCC katika kutoa elimu kwa vikundi hivyo kuhusu athari za bidhaa bandia, ili waweze kulinda shughuli zao na kuwa sehemu ya mapambano haya.” Ameelekeza Mhe. Senyamule 

Pia, ameelekeza waratibu wa vikao vya ushauri vya Mkoa na Wilaya (RCC na DCC) kuhakikisha FCC wanahusishwa katika vikao hivyo ili kutoa elimu na kushiriki kwenye mijadala muhimu inayohusu ushindani na maendeleo ya biashara.

Maadhimisho ya kitaifa ya udhibiti wa bidhaa bandia duniani awali yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo na kufuatiwa na Kongamano la Wafanyabiashara.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA