“TANZANIA SIO SALAMA KWA WAUZAJI, WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” MHE. MAJALIWA

 


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya dawa za kulevya Duniani kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Juni 26, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.





Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA), Aretas Lymo akitoa takwimu za ukamataji wa dawa za kulevya wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumzia jitihada za Mkoa wake kupambana na Dawa za Kulevya wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.







Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Viongozi wengine wa Serikali kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichafanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.










Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikagua mabanda ya maonesho yaliyoshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.








Baadhi ya mashuhuda waliopona baada ya kupata matibabu ya uraibu wa dawa za kulevya walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.






Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea Tuzo ya heshima kwa niaba ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.






Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Dodoma ikiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.








Baadhi ya wananchi walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.








Msanii 'Chid Benz' ambaye pia ni shuhuda wa Uraibu wa dawa za kulevya ambaye anaendelea kuimarika kutokana na matibabu anayoyapata akitumbuiza kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kwenye Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.








Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na makundi tofauti wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya Duniani kilichofanyika katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Juni 26, 2025.





Na. Hellen M. Minja
       Habari – DODOMA RS

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokua akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na biashara ya dawa za kulevya Duniani kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Juni 26, 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Tanzania sio mahali salama kwa wauzaji, wasafirishaji, walimaji n ahata watumiaji wa dawa za kulevya, Tanzania tumeiva na sasa tunaenda kukomesha biashara. Makamishna na Wakuu wa vyombo vya ulinzi, fanyeni kazi, imarisheni ulinzi iwe ni kwenye SGR, vituo vya mabasi, Bandari na Viwanja vya Ndege,mipakani, ili tuweze kuokoa vijana wetu. Dawa hizi zina madhara makubwa kwani zinapoteza uwezo wa mwili na akili”. Mhe. Majaliwa.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA), Bw. Aretas Lymo, amesema katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekamatwa ambapo ni jumla ya kilogram 2,301,411.94 ikilinganishwa na kilogram 2,005,542.73 zilizokamatwa katika awamu zilizopita.

Akitoa salam za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Mkoa wake unaendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kushirikiana na Mamlaka yenye dhamana (DCEA) kwa kufanya oparesheni mbalimbali.

“Tumefanya nao oparesheni kuanzia Julai 2022 mpaka Mei 2025 ambapo tumekamata kilogramu 4335 za Bangi, kilogramu 873 za mirungi na katika kilo hizo, Watuhumiwa 828 wamehusika na kwa kushirikiana nao, tumeweza kudhibiti kwa kuchoma mashamba 645 ya Bangi pia tumetoa elimu inayohusu dawa za kulevya kwa wananchi 136,000”.

 Mwezi Juni kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya Kupiga vita dawa za kulevya, Maadhimisho ambayo hufanyika kwa siku tatu mfululizo (24, 25 na 26) kwa kuhusisha matukio mbalimbali yanayolenga kutoa elimu juu ya madhara ya biashara na matumizi ya dawa hizo hasa kwa rika la vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa. 

#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirthdayyangu



































Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA