VODACOM TANZANIA KUPANDISHA HADHI MINARA YAO KUIMARISHA MAWASILIANO DODOMA

 






Picha tofauti za  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano ya Nje Vodacom Bi. Zuwena Farah walipomtembelea ofisini kwake leo Juni 25, 2025. 





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (katikati) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi (Kulia) na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano ya Nje Vodacom Bi. Zuwena Farah walipomtembelea ofisini kwake leo Juni 25, 2025 kwa lengo la kujitambulisha 








Na. Hellen M. Minja
       Habari – DODOMA RS

Kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom ipo kwenye Mpango wa kuifanyia ukarabati minara yake zaidi ya 50 iliyopo Jijini Dodoma kwa kuipandisha kutoka 3G kwenda 4G na 5G kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kutokana na changamoto za kimawasiliano kwenye maeneo yenye minara ya 3G.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kanda Vodacom Bi. Chiha Nchimbi alipotambulishwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Juni 25 Jijini Dodoma ambapo aliambatana na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano ya Nje Vodacom Bi. Zuwena Farah.

Bi. Nchimbi amesema kuwa zoezi hilo limekuja katika wiki hii ambayo Kampuni hiyo inaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, ambapo wameandaa msafara wa magari yanayo zunguka kwenye Mikoa ya Kanda ya Kati kwa lengo la kukutana na wateja wao na kutoa zawadi mbalimbali.

Sambamba na hilo, msafara huo unaambatana na matukio kadhaa kama vile huduma ya kuuza simu za kupangusa kwa bei ya punguzo, mafunzo kwa Mawakala wa huduma za kifedha (M-Pesa) juu ya mbinu za kufanya biashara kwa kuvutia wateja pamoja na uzinduzi wa minara mipya iliyojengwa kwenye maeneo ya Hombolo na Wilaya ya Mpwapwa.

Mkuu wa Mkoa amemkaribisha Bi. Nchimbi na kuipongeza Kampuni hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wao kwani amekua akipokea taarifa juu ya changamoto ya mawasiliano ya Kampuni hiyo kwenye baadhi ya maeneo hivyo kupitia wiki hii, anaamini changamoto hiyo inakwenda kupatiwa ufumbuzi.


#dodomafahariyawatanzania
#wekezadodomastawishadodoma
#keroyakowajibuwangu
#mtiwangubirhdayyangu










Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA