RC DODOMA AKAGUA MIRADI YA ELIMU KATIKA SHULE YA MSINGI MAYAMAYA, AAGIZA WANAFUNZI WOTE KUREJEA SHULENI
Na Mwandishi wetu Habari - DODOMA RS Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, tarehe 14, Januari 2026 amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Mayamaya iliyopo Wilayani Bahi kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya elimu. Akiwa shuleni hapo, Mhe. Senyamule amesisitiza wajibu wa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha kuwa ndani ya wiki hii wanafunzi wote wanarejea shuleni kuendelea na masomo yao. “Ninaagiza watendaji wa kata na vijiji kupita kaya kwa kaya kuhakikisha kila mwanafunzi anarejea shuleni. Hatupaswi kuwa na mtoto anayebaki nyumbani wakati wenzake wakiendelea na masomo, kwani hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya elimu,” alisema Mhe. Senyamule. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Joachim Nyingo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika Mkoa wa Dodoma, hususan Wilaya ya Bahi na Kata ya Zanka, unaolenga kuboresha sekta ya elimu na maen...