UGENI WA AFYA MALAWI WATUA DODOMA KUJIFUNZA MFUMO WA M-MAMA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya, leo Januari 13, 2026, imepokea ugeni kutoka nchini Malawi.
Ugeni huo, ukiongozwa na Waziri wa Afya wa Malawi, Mhe. Madalitso Baloyi, umetembelea Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa lengo la kujifunza na kujionea utekelezaji wa mfumo wa usafiri wa dharura kwa mama wajawazito, akina mama waliojifungua hadi siku 42, pamoja na watoto wachanga wenye umri wa siku 0–28 (M-MAMA).
Aidha, ugeni huo ulikutana na viongozi wa sekta ya afya pamoja na wadau mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za utoaji wa huduma za afya.
Ujio wa ugeni huu unalenga kuimarisha ushirikiano wa kiafya kati ya Malawi na Tanzania, pamoja na kuchochea ubadilishanaji wa uzoefu miongoni mwa wataalamu wa afya.
Katika ziara hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Thomas Rutachunzigwa, alishiriki kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
#dodomafahariyawatanzania

.jpeg)






.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment