WAZAZI/WALEZI WATAKIWA KUSIMAMIA MAANDALIZI YA KUWAPELEKA WATOTO SHULE
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akizungumza alipokua kwenye shule ya Sekondari Dkt. Samia wakati wa ziara ya kuangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza alipokua kwenye shule ya Sekondari Dkt. Samia wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe kuangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akielekea kwenye madarasa ya shule ya sekondari Dkt. Samia kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari ziara aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa kwenye baadhi ya madarasa ya shule ya sekondari Dkt. Samia kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari ziara aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akikagua Maktaba ya shule ya sekondari Dkt. Samia alipofanya ziara ya kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akielekea kwenye madarasa ya shule ya msingi Iyumbu wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakiwa kwenye moja ya darasa la shule ya msingi Iyumbu wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakiwa kwenye darasa la awali la shule ya msingi Iyumbu wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Mwonekano wa darasa la awali katika shule ya msingi Iyumbu kama lilivyokutwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Iyumbu Monica Nshimba akitoa taarifa ya shule mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Baadhi ya Walimu wa shule ya msingi Iyumbu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari aliyoifanya kwenye shule hiyo na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
Na Mwandishi wetu – DODOMA RS
Wazazi na walezi wametakiwa kusimamia maandalizi ya kupeleka watoto shuleni katika kipindi hiki cha kuanza Muhula Mpya wa masomo Januari 13, 2026 kwani miundombinu iliyopo katika shule za Msingi na Sekondari inaridhisha kujifunza na kujifunzia.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe alipofanya ziara ya kuangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, msingi na sekondari kwenye shule ya msingi Iyumbu na shule ya sekondari Dkt. Samia za Jijini Dodoma Januari 12, 2026.
“Nimeridhishwa na miundombinu iliyopo kwenye shule hii, kazi nyingine ni ya sisi wazazi ambao tumeshawaandikisha watoto au wale ambao bado hatujawaandikisha, na wale waliochaguliwa sekondari, wazazi wahakikishe wanawaleta wanafunzi shuleni.
Aidha, ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata kwenda nyumba hadi nyumba kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule kwenye Kata zao wanakwenda shule, pia Wakuu wa shule za Sekondari wanawapokea wanafunzi waliofaulu na kupangiwa kwenye shule zao.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule aliainisha idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza Muhula Mpya wa Masomo 2026 kwa elimu ya awali kuwa ni 79,131,elimu ya msingi,darasa la kwanza ni wanafunzi 82,569, huku upande wa sekondari, kidato cha kwanza ni wanafunzi 46,453.
Katika taarifa yake, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Iyumbu, Monica Nshimba alisema shule yake ina mazingira mazuri ya kazi kutokana na uboreshaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, sanjari na ujenzi wa madarasa matatu kwa fedha za Halmashauri yaliyoondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.
Nae, Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika shule ya Dkt. Samia Edina Francis, amesema katika Muhula huu mpya, amejipanga kusoma kwa bidii kujiandaa na Mitihani ya Taifa kidato cha sita kutokana na miundombinu bora iliyopo shuleni hapo, huku akitoa hamasa kwa wazazi kuwapeleka watoto wao waliochaguliwa katika shule hiyo.
#DodomaTunatakaAmani
#AmaniYetuUstawiwetu
#WekezaDodomaStawishaDodoma
#KazinaUtuTunasongaMbele






.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


Comments
Post a Comment